• HABARI MPYA

  Jumamosi, Juni 22, 2013

  MH JANUARI YUSSUF MAKAMBA MGENI RASMI MISS TANGA 2013 MKWAKWANI USIKU WA LEO

  Mgeni rasmi; Mh Januari Makamba leo atakuwa mgeni wa heshima Mkwakwania wakati wa Miss Tanga 
  Na Princess Asia, Tanga, IMEWEKWA JUNI 22, 2013 1:00 ASUBUHI
  NAIBU Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Januari Yussuf Makamba, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi leo, katika shindano la kumsaka malkia wa Redd’s Miss Tanga 2013 linalofanyika leo kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini hapa.
  Akizungumza na Waandishi wa Habari mjini hapa jana, Mkurugenzi wa DATK Entertainment, waandaaji wa shindano hilo, Asha Kigundula alisema kwamba maandalizi yamekamilika na wanatarajia shindano litafana.
  Nani kati yao? Washiriki wa Miss Tanga, hapa walikuwa kwenye ziara ya Makamu wa Rais, Dk Mohamed Ghalib Bilal jana wakati wa uzinduzi wa mradi wa uwekezaji eneo la Pongwe, nani atang'ara kati yao?

  “Nashukuru Mungu mambo yamekwenda sawa, kilichokuwa kimesalia ni kumtangaza mgeni rasm na nashukuru
  Tunda Man atatumbuiza
  tumekwishampata tayari Mheshimiwa Makamba na hakuna kingine, cha muhimu Mungu atuongoze katika shughuli yetu mambo yaende sawa,”alisema Asha.

  Aidha, Asha alisema, ameamua kutoa zawadi ya fedha taslimu kwa warembo na sio vitu, ili warembo wake waweze kupata fursa ya kujichagulia kitu cha kununua
  wenyewe kuliko kununuliwa.
  Alisema Mshindi wa kwanza ataondoka na kitita cha Sh 500,000, wa pili 300,000 na wa tatu 250, 000, wakati wa nne na wa tano kila mmoja atapata Sh. 200, 000 na warembo wengine watakaosalia watapata Sh 100,000 kila mmoja kama kifuta jasho na kutakuwa na zawadi pia kwa mrembo mwenye nidhamu zaidi.
  Kama Makomandoo; Hapa walikuwa kwenye ziara ya mapango ya Amboni
  Alisema pia kutakuwa na zawadi kwa mrembo mwenye nidhamu ili kuweza kuboresha shindano hilo na kwa upande wa burudani msanii nyota nchini, Tunda Man kutoka Tip Top Connection, ataongoza idara hiyo akipewa tafu na wasanii wengine kibao kama Rapa wa lililokuwa kundi la Wagosi wa Kaya, Dk. John, Nabisha kutoka THT, Fady Dady na wasanii chipukizi kutoka mkoani hapa.
  Alisema shindano hilo linatarajiwa kuanza majira ya saa 2:00 usiku na kushirikisha warembo 12, ambao watachuana pamoja na kuwania Umalkia wa mkoa huu, lakini pia kuwania moja ya nafasi tatu za kuiwakilisha Tanga katika shindano la ngazi ya kanda.
  TBL; Hapa walikuwa kwenye ziara ya Kampuni ya Bia (TBL), tawi la Tanga

  Warembo wanaotarajiwa kuchuana leo ni Hawa Ramadhani (18), Hazina Mbaga (19), Like Abdulraman (19), Irene Thomas(20), Tatu Athumani (19), Winfrida Gutram (21), Lulu Mbonela (19), Hazina Daniel (19), Lulu Matawalo(22), Judith Molel (21), Neema Jonas na Hawa Twaybu(21).
  Walipata bia pia; Hapa walialikwa chakula cha jioni na kinywaji kidogo

  Shindano la Redd’s Miss Tanga 2013 limedhaminiwa na BIN ZUBEIRY Blog, Al Hayat Investment Limited, Dodoma Wine, CXC Africa, Executive Solutions, Busta General Supply, Mkwabi Enterprises, Lusindic Investment LTD, Lavida Pub, Jambo Leo, Staa Spoti, Five Brothers, Cloud's Media Group, Michuzi Media Group, Saluti5, Kajuna, JaneJohn, Kidevu na assengaoscar.blogspot.com.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: MH JANUARI YUSSUF MAKAMBA MGENI RASMI MISS TANGA 2013 MKWAKWANI USIKU WA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top