• HABARI MPYA

  Alhamisi, Juni 27, 2013

  REAL MADRID YATAMBA KUIPIGA BAO LA KISIGINO MAN CITY...ISCO ANATUA BERNABEU

  IMEWEKWA JUNI 27, 2013 SAA 7:00 MCHANA
  RAIS wa Real Madrid, Florentino Perez amesema kwamba klabu yake imekubaliana na Malaga dili la kuikosesha Manchester City mchezaji wanayemtaka, Isco ambaye sasa atahamia Bernabeu.
  Isco, mwenye umri wa miaka 21, kwa muda mrefu amekuwa akihusishwa na kuhamia Madrid na kuwasili kwa kocha mpya, Carlo Ancelotti, ambaye alitambulishwa kuwa mrithi wa Jose Mourinho jana, ni mwanzo wa kukamilika kwa uhamisho wake.
  Gazeti la Hispania, AS limenukuu Perez akiiambia Radio Nacional: "Kuna makubaliano baina ya klabu na mchezaji.
  Wanted: Isco has previously admitted he is excited by the prospect of joining Real Madrid
  Anayetakiwa: Isco awali alisema anavutiwa kuhamia Real Madrid
  Champion: Isco starred in Spain's victorious run to winning the U21 European Championships
  Bingwa: Isco alikuwemo kwenye kikosi cha Hispania cha vijana chini ya miaak 21 kilichotwaa ubingwa wa Ulaya

  "Atatambulishwa wiki ijayo baada ya vipimo vya afya,".
  Taarifa nchini Hispania zinasema ada ya uhamisho itakuwa ni Euro Milioni 27.
  Real pia inamtaka mshambuliaji wa Tottenham, Gareth Bale, huku Cristiano Ronaldo akiwa hatarini kuondoka.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: REAL MADRID YATAMBA KUIPIGA BAO LA KISIGINO MAN CITY...ISCO ANATUA BERNABEU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top