• HABARI MPYA

  Jumatano, Juni 26, 2013

  RONALDO KUKUTANA FARAGHA NA VIONGOZI MAN UNITED...SAFARI YA KUREJEA OLD TRAFFORD IMEIVA

  IMEWEKWA JUNI 26, 2013 SAA 4:10 USIKU
  MRENO Cristiano Ronaldo anaweza kurejea Manchester United baada ya kugundulika atakuwa na mkutano na viongozi wa klabu hiyo ya Old Trafford ndani ya siku tatu zijazo. 
  Nyota huyo wa Real Madrid amekuwa akihusishwa na kurejea England baada ya kupitia msimu wa bila furaha Bernabeu, lakini ilitarajiwa kuwasili kwa kocha mpya, Carlo Ancelotti kungemfanya abaki Hispania. 
  Na gazeti la Hispania, El Pais limeripoti kwamba nahodha huyo wa Ureno atakutana na viongozi wa United, kabla hajaenda kuanza maandalizi ya msimu mpya Madrid.
  Transfer saga: If United persuade Ronaldo to return it would surely be the move of the summer
  Transfer saga: If United persuade Ronaldo to return it would surely be the move of the summer
  Sakata la kuhama: Ikiwa United itafanikiwa kumnasa Ronaldo, utakuwa usajili babu kubwa zaidi majira haya ya joto

  JINSI ALIVYOKUWA MTAMBO WA MABAO

  Manchester United 
  LIGI: Mechi 196, mabao 84
  KOMBE: Mechi 38, mabao 17
  ULAYA: Mechi 55, mabao 16
  JUMLA: Mechi 189, mabao 117
  Real Madrid 
  LIGI: Mechi 135, mabao 146
  KOMBE: Mechi 20, mabao 17
  ULAYA: Mechi 40, mabao 35
  JUMLA: Mechi 195, mabao 198
  Kwa kuwa FIFA inazuia klabu kufanya mazungumzo na wachezaji walio ndani ya Mikataba na klabu zao, pande zote zimejipanga kukana kufanya mazungumzo, ambayo itamsaidia sana kocha mpya, David Moyes kuelekea msimu ujao.
  Lakini Ancelotti amesema wakati akitambulishwa kuwa kocha mpya wa Madrid leo kwamba: "Cristiano ni mchezaji mkubwa na ninajivunia kufanya naye kazi. 
  "Nimewakochi Zidane, Ronaldo na Ronaldinho, na ninajivunia kumuongeza na yeye.' 
  Alipoulizwa kuhusu Radamel Falcao, mchezaji aliyekuwa anawaniwa na Madrid ambaye amesaini Monaco, Ancelotti alisema: "Ni mchezaji mzuri, lakini kuna Ronaldo, Higuain na Benzema,"alisema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: RONALDO KUKUTANA FARAGHA NA VIONGOZI MAN UNITED...SAFARI YA KUREJEA OLD TRAFFORD IMEIVA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top