• HABARI MPYA

  Alhamisi, Juni 20, 2013

  NEYMAR AISAIDIA SANA TU BRAZIL KUIFUMUA MEXICO 2-0 USIKU HUU

  IMEWEKWA JUNI 20, 2013 SAA 7:30 USIKU
  TIMU ya taifa ya Brazil imeshinda mechi yake ya pili ya Kombe la Mabara, huku kijana mdogo mwenye kipaji cha ajabu, Neymar akifunga bao tamu ndani ya dakika 10 za kwanza kabla ya kumtengenezea nafasi ya kufunga bao la pili Jo.
  Brazil imeilaza Mexico mabao 2-0 bila ubishi na sasa inatimiza ponti sita na kuzidi kujiimarisha kileleni mwa Kundi A.
  Daniel Alves alipinda krosi kutoka kulia na nyota mpya wa Barcelona, Neymar akaitokea wa kwanza mbele ya beki wa Mexico, kabla ya kuhadaa na kumtungua kipa Jose Corona dakika ya tisa na dakika ya 90 akampa pande Jo kufunga la pili.
  Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Howard Webb wa Uingereza, kikosi cha Brazil kilikuwa: Cesar, Alves, Silva, Luiz, Marcelo, Luiz Gustavo, Paulinho, Oscar/Hernanes dk62, Hulk/Lucas Moura dk78, Neymar na Fred. 
  Mexico: Corona, Rodriguez, Salcido,  Torrado, Dos Santos, Henandez, Moreno,  Guardado, Torres/Barrera dk70, Mier na Flores/Herrera dk68.  
  Smashing: Neymar scored the only goal of the game for Brazil after his first-half volley
  Balaa: Neymar alikuwa shujaa wa Brazil leo
  Jubilation: Neymar celebrates his goal with the other Brazil players
  Pongezi: Neymar akishangilia bao lake
  Upended: Javier Hernandez goes down under a challenge from Thiago Silva
  Javier Hernandez akiwa chini baada ya kukutana na shuluba la Thiago Silva
  Ouch! David Luiz had a clash of heads with centre-back partner Thiago Silva
  Damu! David Luiz aliumizwa kichwani na beki mwenzake wa kati, Thiago Silva hadi kutokwa damu
  Bloody nose: Luiz was looking groggy went he got sat up after the challenge
  Luiz akitibiwa
  Pants: The blood resulted in a rapid change for kit for the Chelsea man
  Damu ilisababisha abadilishe jezi
  Running: Neymar tries to get away from Mexico's Gerardo Torrado
  Mbio: Neymar akijaribu kumtoka Gerardo Torrado wa Mexico
  Chasing: Hulkl competes with Jorge Torres Nilo of Mexico
  Hulkl akipambana na Jorge Torres Nilo wa Mexico
  Full of support: Brazil fans were out in their numbers in Fortaleza
  Shabiki wa Brazil 
  In agony: Neymar was trying to have more of an influence in the game, but sometimes to his peril
  Neymar akiugulia maumivu katika moja ya matukio ya mechi hiyo baada ya kuumia
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: NEYMAR AISAIDIA SANA TU BRAZIL KUIFUMUA MEXICO 2-0 USIKU HUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top