• HABARI MPYA

  Ijumaa, Juni 28, 2013

  MAN UNITED KUMPANDIA DAU BAINES HADI PAUNI MILIONI 20

  IMEWEKWA JUNI 28, 2013 SAA 11:28 ALFAJIRI
  KLABU ya Manchester United itampandia dau beki wa Everton, Leighton Baines hadi Pauni Milioni 15. 
  Baada ya kuipiga chini ofa yao ya awali ya Man United ya Pauni Milioni 12, Everton imesema beki huyo wa kushoto wa kimataifa wa England hauzwi.
  Lakini United imepania kupanda dau hadi Pauni Milioni 20 katika kuwania saini ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28.
  Next stop, Manchester: Moyes will be looking to install Baines as United's first-choice left-back
  Atatua, Manchester? David Moyes anamtaka Baines awe chaguo lake la kwanza katika beki ya kushoto
  Main man: David Moyes wants to bring reliable left-back Leighton Baines to Manchester United
   
  Mrithi wa Moyes, Everton, Roberto Martinez anataka kumbakzia beki huyo mwenye thamani ya Pauni Milioni 20 na klabu hiyo inataka kumpa Mkataba mpya ikimuongezea mshahara hadi Pauni 70,000 wiki.
  Mwenyekiti wa Everton, Bill Kenwright alielezea umuhimu wa Baines kwao, akisema: "Leighton ana Mkataba na nimemuambia David usimfuate tena, ingawa hakuna cha kumzuia. Anajua tunataka abaki,". 
  Mpango huu unamuweka shakani beki Mfaransa, Patrice Evra juu ya mustakabali wake Old Trafford na wazi sasa anaweza kuhamia Monaco au Paris Saint-Germain. 
  David Moyes
  Patrice Evra
  Nia: Mpango wa Moyes kutaka kumsajili beki wa Everton, Baines unaleta shaka juu ya mustakabali wa Patrice Evra
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: MAN UNITED KUMPANDIA DAU BAINES HADI PAUNI MILIONI 20 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top