• HABARI MPYA

  Jumatatu, Juni 24, 2013

  KONE SASA AGOMBEWA NA LIVERPOOL, EVERTON, NOWRICH NA CRYSTAL

  IMEWEKWA JUNI 24, 2013 SAA 1:00 ASUBUHI
  KOCHA wa Norwich, Chris Hughton anapambana kuipiga bao Everton katika kuwania saini ya mshambuliaji wa Wigan, Arouna Kone
  Mkataba wa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast ua thamani ya Pauni Milioni 5. Msimu uliopita amefunga mabao 13 na kuisaidia Wigan kutwaa Kombe la FA. Hull, Liverpool na Crystal Palace zote zinamtaka pia.
  Arouna Kone and Roberto Martinez
  Uwezekana wa kuungana tena: Wakiwa wametwaa Kombe la FA pamoja Wigan msimu uliopita, Arouna Kone (kushoto) anaweza kuungana tena na kocha mpya wa Everton, Roberto Martinez (kulia).

  Jumapili, Kone alizipigia kengele klabu kubwa baada ya kusema hayuko tayari kucheza Daraja la Kwanza, kufuatia Wigan kushuka daraja.
  Akizungumza na The Sun, nyota huyo wa zamani wa PSV Eindhoven alisema: "Wakati wote una malengo kama mchezaji, na siko tayari kucheza ligi ya pili England.
  "Wigan imeshuka, ambayo ni aibu kubwa. Ni juu yao kuweka mambo sawa juu ya mipango yangu. Mimi ni wa kucheza moja ya klabu bora England,  na natumai nitapata nafasi.
  Kone alikuwa Dar es Salaam wiki mbili zilizopita kuichezea Ivory Coast dhidi ya wenyeji, Tanzania

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: KONE SASA AGOMBEWA NA LIVERPOOL, EVERTON, NOWRICH NA CRYSTAL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top