• HABARI MPYA

  Ijumaa, Juni 21, 2013

  NIGERIA YAPIGWA KOMBE LA MABARA, NI KAMA IMEKWISHATOLEWA TU

  IMEWEKWA JUNI 21, 2013 SAA 12:00 ASUBUHI
  MSHAMBULIAJI Diego Forlan usiku wa kuamkia leo amesherehekea mechi yake ya 100 Uruguay kwa kufunga bao la ushindi timu yake ikishinda 2-1 dhidi ya Nigeria kwenye Kombe la Mabara mjini Salvador.
  Forlan alifunga mwanzoni mwa kipindi cha pili baada ya John Obi Mikel kuisawazishia Nigeria dakika ya 37 kufuatia Uruguay kufunga bao la kuongoza dakika ya 19 kupitia kwa Diego Lugano.
  Snatched: Forlan bagged the winner for Uruguay in their second group game
  Forlan akishangilia na mwenzake
  Ahead: Uruguay's Diego Lugano is congratulated after scoring the opening goal
  Diego Lugano akipongezwa na wenzake
  Uruguay
  Matokeo hayo yanafanya timu mbili katika Kundi hilo, B zilingane kwa pointi, tatu kila moja baada ya kucheza mechi mbili, lakini ikiwa imebakiza mechi na Tahiti, Uruguay iko katika nafasi kubwa ya kusonga mbele pamoja na Hispania, yenye pointi sita na itacheza na Nigeria katika mechi ya mwisho ya kundi hilo.

  KUNDI B KOMBE LA MABARA

  TimuMechiKushindaSareKufungwaMabao ya KufungwaMabao ya kufungwaPointi
  Hispania22001216
  Nigeria2101733
  Uruguay2101333
  Tahiti20021160
  Level: Nigeria's John Obi Mikel (right) celebrates after scoring the equaliserscoring
  John Obi Mikel (kulia) akishangilia baada ya kufungaStuck in: Martin Caceres of Uruguay challenges Ahmed Musa
  Martin Caceres wa Uruguay akimdhibiti Ahmed Musa
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: NIGERIA YAPIGWA KOMBE LA MABARA, NI KAMA IMEKWISHATOLEWA TU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top