• HABARI MPYA

    Tuesday, June 18, 2013

    ULAJI HUOO, KLABU THAILAND YASAKA WACHEZAJI TANZANIA WAKACHEZE ULAYA

    Huyu vipi; Mbwana Samatta anacheza TP Mazembe ya DRC, je atakubali kuhamia Thailand ajitengenezee mazingira ya kwenda Ulaya?
    Na Boniface Wambura, IMEWEKWA JUNI 18, 2013 SAA 12:50 JIONI
    KLABU ya Thai Port Football ya Thailand inatafuta wachezaji nchini Tanzania kwa ajili ya kucheza soka nchini humo na katika nchi nyingine barani Ulaya.
    Kupitia kwa wakala wake, klabu hiyo imetuma taarifa kupitia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ikitaka wachezaji wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 28 kwa ajili ya kuwafanyia majaribio ambapo watakaofuzu watacheza nchini humo na katika klabu nyingine za Ulaya ambazo wana ushirikiano nazo.
    Wachezaji wenye nia ya kufanya majaribio wanatakiwa kutuma taarifa za wasifu wao (CV) kwa klabu hiyo kwa njia ya emaili, wawe na pasi ya kusafiria pamoja na pasi ya mchezaji (player passport).
    Wakala atapitia vitu hivyo, na kwa wachezaji atakaowahitaji atawatumia tiketi za ndege na viza kwa ajili ya kwenda kufanya majaribio nchini humo, na watakaofanikiwa kabla ya kusaini nao mikataba watawasiliana na klabu zao nchini (kwa wale wenye klabu).
    Katika hatua nyingine, TFF inawashukuru washabiki kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Taifa Stars na Ivory Coast (The Elephants) iliyochezwa juzi (Jumapili) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Mwitikio wa washabiki katika mechi hiyo ilikuwa ni moja ya chachu ya kiwango kilichoonyeshwa na Taifa Stars, kwani walishangilia mwanzo hadi mwisho licha ya kupoteza kwa mabao 4-2.
    Ni matarajio utakuwepo mwitikio kama huo huo katika mechi ijayo ya Taifa Stars ya michuano ya Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Nyumbani (CHAN) dhidi ya Uganda (The Cranes) itakayochezwa Dar es Salaam kati ya Julai 12-14 mwaka huu. Stars itaingia tena kambini Julai 4 mwaka huu kujiandaa kwa mechi hiyo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: ULAJI HUOO, KLABU THAILAND YASAKA WACHEZAJI TANZANIA WAKACHEZE ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top