• HABARI MPYA

  Jumanne, Juni 25, 2013

  CHELSEA YAFIKA BEI KWA CAVANNI, NAPOLI YATANGAZA KATIKA REDIO YAKE INAMUUZA DARAJANI PAUNI MILIONI 49 NA UPUUZI

  IMEWEKWA JUNI 25, 2013 SAA 1:00 ASUBUHI
  KITUO cha Redio cha Napoli, Marte kimetangaza kwamba dau la Pauni Milioni 49.3 limetolewa na Chelsea kwa ajili ya mshambuliaji  Edinson Cavani.
  Katika taarifa ya jana usiku, Radio Marte ilitangaza: "Tumepokea taarifa kutoka ofisini kwa vyanzo vya kuaminika kwamba, Napoli imekubaliana dili la kuiuzia Chelsea Cavani.
  Hot shot: Chelsea appear to be in pole position to sign Edinson Cavani
  Kitu moto: Chelsea sasa ipo katika nafasi ya kumnasa Edinson Cavani

  "Rafa Benitez pia amebariki, lakini kabla ya kutangaza rasmi, Napoli inataka kupata mshambuliaji atakayeziba pengo la Il Matador.
  "Aurelio De Laurentiis", klabu itasomba kiasi cha Euro Milioni 58, sawa na dili la Ezequiel Lavezzi kwenda PSG mwaka jana.
  "Mchezaji huyo atajiingizia mshahara wa Euro Milioni 8.5 kwa msimu pamoja na haki za picha,". Habari zimevuja kama kwamba Cavani ametangaza anataka kukutana uso kwa uso na Rais, Aurelio de Laurentiis na kuna taarifa kwamba Manchester United nayo imo kwenye mbio hizo. 
  Mshambuliaji huyo wa Uruguayna baba yake awali walionyesha nia ya kutaka kwenda Real Madrid. Klabu hiyo ya Hispani iliwasiliana na Napoli, lakini sasa itabidi waipiku ofa iliyotolewa na Chelsea.
  Most wanted: Man United and PSG are also keeping tabs on Cavani
  Anayetakiwa sana: Man United na PSG pia zinamtaka Cavani
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: CHELSEA YAFIKA BEI KWA CAVANNI, NAPOLI YATANGAZA KATIKA REDIO YAKE INAMUUZA DARAJANI PAUNI MILIONI 49 NA UPUUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top