• HABARI MPYA

    Saturday, June 15, 2013

    MKUU WA WILAYA TANGA AFAGIA BARABARA NA MABINTI WA KITANGA

    Mwanamke Usafi; Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dandego akiwaongoza warembo wanaoshiriki Miss Tanga kufanya usafi  

    Na Asha Said, Tanga, IMEWEKWA JUNI 15, 2013 SAA 7:20 MCHANA
    MKUU wa wilaya ya Tanga,Halima Dendego amemtaka mrembo atakayochaguliwa katika shindano la kumtafuta malkia wa Mkoa wa Tanga,Redd’S Miss Tanga 2013 kuhakikisha anautangaza vema uzuri wa mkoa wa Tanga na vivutio vyake ili kuweza kuwapa uelewa wananchi wengine kuufahamu mkoa wa Tanga.
    Shindano hilo linatarajiwa kufanyika katika uwanja wa Mkwakwani Jumamosi ijayo ya June 22 mwaka huu ambalo litasindikizwa na wasanii nguli wa mziki wa bongofleva hapa nchini.
    Dendego alitoa kauli hiyo jana wakati akifanya usafi na warembo hao katika barabara ya Taifa ambapo warembo wanaowania taji hilo walishiriki zoezi hilo ambalo hufanyika kila Jumamosi mkoani Tanga lenye lengo la kuuweka mji katika mazingira mazuri maarufu kama “Kalembo Day”
    Alisema ushiriki wao katika zoezi hilo wanaonyesha ni jinsi gani warembo hao walivyokuwa karibu na jamii ambazo zinawazunguka na kuwataka kuendelea kuhamasisha na wanajamii wengine ili nao waweze kushiriki katika usafi kwa ajili ya kuyaweka maeneo yao kwenye muonekano mzuri.
    Aidha alisema amefarijika sana kushiriki katika zoezi hilo na warembo hao na kuelezea kuwa shindano hilo litakuwa na upinzani mkubwa kutokana na warembo bombo ambao wanawania taji hilo ambalo hufanyika kila mwaka mkoani hapa.
    Mkuu huyo wa wilaya aliwaomba wakazi wa mkoa wa Tanga kujitokeza kwa wingi kuweza kushuhudia shindano hilo ambalo limesheheni warembo wakali na kuona jinsi washiriki hao watakavyo fanya maonyesho mbalimbali kabla ya kuanza kinyang’anyiro hicho.
    Kwa upande wake,Mratibu wa Redd’s Miss Tanga 2013,Asha Kigundula ambaye ni Mkurugezi wa Kampuni ya DATK Intertaimeint, Asha Kigundula,alimpongeza Mkuu huyo wa wilaya kwa kuona umuhimu wa kushiriki zoezi hilo na kuwataka wakazi wa mkoani wa Tanga kutoka wilaya zote kujitokeza kushuhudia shindano hilo ambalo litakuwa la aina yake.
    Kigundula alisema maandalizi ya shindano hilo yanaendelea vizuri na zawadi za washindi zitatangazwa Jumatano wiki ijayo huku warembo wanaowania shindano hilo kila mmoja akionekana kutamba kuchukua taji hilo ambalo linaonekana litakuwa na upinzani mkubwa.
    Hawa Ramadhani ambaye ni mmoja kati ya washiriki wa shindano hilo alisema suala la usafi ni muhimu hasa katika jamii za watanzania na kuwataka waendelee kuhakikisha wanafanya hivyo kila wakati ili kuyaweka mazingira yao mazuri na salama kwa wageni na wenyeji.
    Kwa upande wake,Mwalimu wa warembo hao,Mariam Bandawe alisema wameanza kufanya zoezi hilo la usafi ili kuweza kuonyesha mfano kwa wananchi wa mkoa wa Tanga kwa sababu usafi ni muhimu. 
    Warembo hao ni Hawa Ramadhan (18),Hazina Mbaga (19)Like Abdulraman (19), Wahida Hashimu(20), Tatu Athumani (19), Winfrida Gutram (21)Lulu Mbonela (19) ,Hazina Daniel (19),Lulu Matawalo(22),Judithi Moleli (21) na Hawa Twaybu(21)
    Redd's, Miss Tanga, imedhaminiwa na BIN ZUBEIRY Blog, Dodoma Wine, CXC Africa, Executive Solutions, Busta General Supply, Mkwabi Interprises, Lusindic Investment LTD, Lavida Pub, Jambo Leo, Staa Spoti, Five Brothers, Cloud's Media Group, pamoja na Blog Michuzi Media Group, Saluti5, Kajuna, JaneJohn, Kidevu na assengaoscar.
    Mwanamke mazingira babu weee!
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MKUU WA WILAYA TANGA AFAGIA BARABARA NA MABINTI WA KITANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top