• HABARI MPYA

  Ijumaa, Juni 21, 2013

  MISS TANZANIA AVUA TAJI MISS KINONDONI LEO

  Mkurugenzi wa Miss Tanzania, Hashimu Lundenga kulia akiwa na washiriki wa Miss Kinondoni
  Na Mwandishi Wetu, IMEWEKWA JUNI 21, 2013 SAA 12:20 ASUBUHI
  REDD’S Miss Tanzania, Brigette Alfred leo anatarajiwa kuvua taji jingine, pale kutakapokuwa na kinyang’anyiro kikali cha kumsaka Redd’s Miss Kinondoni.
  Shindano hilo linalotarajiwa kufanyika katika hoteli ya Golden Tulip, Dar es Salaam linasubiriwa kwa hamu kubwa ili kujua nani atarithi mikoba ya Brigette.
  Mrembo huyo alianza kuvua rasmi mataji yake wakati wa shindano la Redd’s Miss Sinza na sasa ni wakati mwingine wa kukabidhi taji la Redd’s Miss Kinondoni ambalo analishikilia.
  Akizungumzia shindano hilo, Mratibu wa Redd’s Miss Kinondoni, Dennis Ssebo alisema kila kitu kimekamilika na warembo wote wako tayari kwa ushindani mkubwa ulio mbele yao.
  Jana wajumbe wa Kamati ya Redd’s Miss Tanzania walitembelea kambi ya warembo hao iliyopo katika hoteli ya JB Bellmont ili kuwatia moyo.
  Alipoulizwa kuhusu shindano hilo, Brigette alisema ana uhakika mkubwa Redd’s Miss Tanzania mwaka huu atatoka Kinondoni pia.
  Washindi wane kutoka Redd’s Miss Kinondoni watapata fursa ya kuingia moja kwa moja katika shindano la Redd’s Miss Tanzania litakalofanyika baadaye mwaka huu.
  Wakati Kinondoni wakisaka mrembo wao, kazi nyingine kubwa itakuwa kesho katika kumpata Redd’s Miss Tanga shindano ambalo litafanyika katika Uwanja wa Mkwakwani, mjini humo.
  Mratibu wa shindano hilo, Asha Said alisema kutakuwa na burudani kubwa itakayotolewa na wasanii mbalimbali wakiwemo Tunda Man, Nabisha kutoka THT na Fady Dady. Kiingilio katika shindano hilo kitakuwa Sh 15,000 kwa viti maalumu na Sh 5,000 kwa vile vya kawaida.
  Shindano la Redd’s Miss Tanzania kwa sasa linadhaminiwa na kinywaji cha Redd’s Original kinachozaliswa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: MISS TANZANIA AVUA TAJI MISS KINONDONI LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top