• HABARI MPYA

  Jumamosi, Juni 22, 2013

  TOMEKA NDIYE MISS KINONDONI 2013

  Lucy Tomeka katikati akiwa na washindi wake wa pili, Prisca Clement kulia na mshindi wa tatu  Philion Lemi
  Na Prince Akbar, IMEWEKWA JUNI 22, 2013 SAA 8:00 MCHANA
  KUMEKUCHA! Redd’s Miss Tanzania, Brigitte Alfred ameendelea kuvua mataji yake baada ya juzi usiku kumkabidhi taji la Redd’s Miss Kinondoni,  Lucy Tomeka katika shindano lililofanyika ukumbi wahoteli ya Golden Tulip, Dar es Salaam.
  Kwa sasa Brigitte, amebakiwa na taji moja tu la Redd’s Miss Tanzania baada ya kuvuliwa jingine la Redd’s Miss Sinza wiki mbili zilizopita.
  Katika shindano hilo lililovuta hisia za watu, kulikuwa na ushindani mkubwa kutoka kwa warembo 12 walioshiriki katika kinyang’anyiro hicho, kilichoambatana na burudani kibao.
  Warembo waliofanikiwa kuingia katika tano bora walikuwa ni Lucy Tomeka, Prisca Clement, Phillios Lemi, Sarah Paul na Linda Joseph na hivyo kuwaweka roho juu mashabiki kutojua nani atatwaa taji.
  Katika shindano hilo nafasi ya pili ilikwenda kwa Prisca Clement, akifuatiwa na Phillios Lemi, hivyo kutoa fursa kwa washindi hao kuingia moja kwa moja katika shindano la Redd’s Miss Tanzania.
  Kinyang’anyro cha Redd’s Miss Tanzania kwa sasa kinadhaminiwa na kinywaji cha Redd’s Original kinachozalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: TOMEKA NDIYE MISS KINONDONI 2013 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top