• HABARI MPYA

  Jumatano, Juni 26, 2013

  MAKUMBUSHO MABINGWA AIRTEL RISING STARS KINONDONI
  Nahodha wa timu ya Makumbusho United, Hamza Mohamed akipokea Kombe la ubingwa wa Airtel Rising Stars, mkoa wa Kinondoni.
  Na Prince Akbar, IMEWEKWA JUNI 26, 2013 SAA 5:30
  TIMU ya Makumbusho United imetawazwa kuwa bingwa wa Airtel Rising Stars mkoa wa kisoka wa Kinondoni baada ya kuwafunga bila huruma Mtakuja Beach 5-1 katika mchezo wa fainali wa mashindano hayo ya vijana chini ya umri wa miaka 17 Uwanja wa shule ya Msingi Mwananyamala, Dar es Salaam jana.
  Mabingwa hao wapya wa ARS ngazi ya mkoa walianza michuano hiyo kwa kishindo walipoitandika Sifa United 3-1 katika mchezo wa ufunguzi uliopigwa katika uwanjwa huo huo Jumapili. Katika mchezo wa leo, Makumbusho wamepata magoli kupitia kwa Premji Stephano (dk 12), Ally Amin (dk 35), Rashid Ngone (dk 38 na 71) na  Wllie Kalolo (dk 53) wakati Mtakuja walipata goli la kufutia machozi dakika ya 78 kwa njia ya penati iliyopigwa na Steven Munyu.
  Jijini Mbeya, timu ya Mbasco ilitoshana nguvu na timu ya Mbosa Jumatatu Juni 24 baada ya kutoka sare ya 3-3 katika mchezo wa vuta nikuvute wa Airtel Rising Stars. Mbasco walipata magoli yao kupitia kwa Jasco Mwaibabe (dk 20 na 50) na Joel Kasimila dakika ya 68. Mchezo huo ulifanyika kwenye kiwanja cha Magereza Mbeya.
  Kwa upande wao, Mbosa walipata magoli yao kupitia kwa Michael Mwashilanga (dk 5), Richard Kalinga (dk 49) na Enock Chikaonga (dk 9).
  Mjini Morogoro; timu ya Moro kids iliishinda Anglikana 3-0 katika mchezo mwingine wa Airtel Rising Stars ngazi ya mkoa uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya seconday ya Morogoro. Magoli ya Moro kids yaliwekwa kimiani na Abdul Rashid, Robert Nashon na Evans Nashon. Robert na Evans ni mapacha.
  Katika mkoa wa kisoka wa Ilalan, Msimamo Youth Academy walipata ushiindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Buguruni Youth Center katika mchezo mgumu iliofanyika kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam. Goli hilo la ushindi lilifungwa dakika za majeruhi na nahodha wa timu hiyo Rajab Mohamed katika dakika ya 89
  Mkoa wa kisoka waTemeke ulitarajiwa kuanza mechi zake za Airtel Rising Stars ngazi ya mkoa jana (leo) katika uwanja wa Twalipo na mkoa wa Mwanza vile vile ulitarajia kuanza mechi zake kwenye uwanja mkongwe wa Nyamagana jana (leo). 
  Programu hii ya Airtel Rising Stars ni ya Afrika nzima likiwa na lengo la kuendeleza na kukuza  mpira wa miguu katika bara la Afrika kwa vijana wanaochipukia waweze kupata nafasi ya kuendeleza vipaji vyao.
  Fainali za ARS Taifa vile vile zitatumika kuchagua timu bora za wavulana na wasichana ambao wataiwakilishaTanzania katika mashindano ya kimataifa ambapo nchi mwenyeji wa michuano hiyo itatangazwa mwezi ujao. Wachazeaji wengine watachaguliwa kwenda kwenye kliniki itakayoendeshwa na makocha kutoka klabu maarufu duniani ya Manchester United
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: MAKUMBUSHO MABINGWA AIRTEL RISING STARS KINONDONI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top