• HABARI MPYA

  Jumapili, Juni 23, 2013

  LULU AMBONEA NDIYE MISS TANGA 2013, ILA MAJAJI...

  Miss Tanga 2013, Lulu Ambonea akiwa na washindi wake wa pili, Like Kipenga na mshindi wa tatu Hawa Ramadhani.
  Na Princess Asia, Tanga IMEWEKWA JUNI 23, 2013 SAA 9:00 USIKU
  KIMWANA Lulu Ambonea aliyezaliwa miaka 20 iliyopita, usiku huu ametwaa taji la Miss Tanga 2013 katika shindano lililofanyika kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga na kujinyakulia kitita cha Sh. 500,000 na tiketi ya kushirki shindano la Kanda ya Kaskazini kuelekea Miss Tanzania mwaka huu.
  Katika shindano hilo, binti wa kipa wa zamani wa Pilsner ya Dar es Salaam, Abdulrahman Kipenga, aitwaye Like, alikamata nafasi ya pili na kujinyakulia Sh. 300,000 na tiketi ya Kanda, wakati mshindi wa tatu alikuwa Hawa Ramadhani, aliyepata 200,000 na tiketi ya Kanda.
  Winfrida Gutram hakuingia tano bora


  Irene Thomas hakuingia tano bora 

  Miss Talent Hazina Daniel hakuingia tano bora pia

  Mrembo Asia Rashid akishindana wakati wa Talent. Shabiki huyu alipanda kumtuza
  Warembo wengine wawili walioingia tano bora ni Hawa Twalib na Judith Molel ambao kila mmoja alipata Sh. 100,000 na safari yao inaishia Mkwakwani.
  Washiriki wengine saba, kila mmoja alipata Sh. 100,000 wakati mshindi wa taji la Miss Talent, Hazina Daniel alipata 100,000 zaidi kwa kushinda taji hilo.
  Hata hivyo, majaji wa shindano hilo walijikuta katika wakati mgumu baada ya kuzomewa na watazamaji kutokana na imani kwamba wameboronga.
  Tunda Man akitumbuiza


  Asha Kigundula akikabidhi cheti cha shukrani kwa Bin Zubeiry

  Familia ya Bin Zubeiry ilikuwepo Mkwakwani

  Miss Tanga wa watazamaji; Hazina Daniel alishangiliwa sana na watazamaji, wakisema ndiye Miss Tanga 

  Hali hiyo ilijitokeza wakati wa kutajwa wasichana walioingia tano bora na Jaji Mkuu, Boniface Shelufumo alipowataja mabinti walioingia hatua hiyo alizomewa akiambiwa wamependelea.
  Imani ya watazamaji ilikuwa kwamba kuna wasichana waliostahili kuingia tano bora, lakini wamechujwa na walioingia hawakuwa bora zaidi ya walioachwa.
  Hali hiyo ilimvunja nguvu Jaji Mkuu huyo na kujikukuta anatetemeka kila alipopanda jukwaani na kutangaza kwa makosa, mfano Lulu alimtaja kama mshindi wa tatu wakati ndiye Miss Tanga kabla ya kurekebisha wakati akiwa tayari amevishwa taji la mshindi wa tatu.
  Msimamizi wa shindano, Ricco akiwakoromea majaji. Katikati ndiye alikuwa Jaji Mkuu 


  Asha akimkabidhi cheti Mkuu wa Wilaya, Hawa Dendegu

  Akimkabidhi Swedi Nkwabi

  Jamaa akienda kutuza dola kwa mrembo

  Dk John akitumbuiza

  Hali hiyo ilionekana kumkera hata na Msimamizi wa shindano hilo kutoka Kamati ya Miss Tanzania, Hiddan Rico ambaye alikuwa akimsogelea mara kadhaa jaji wake huyo kumsahihisha jukwaani hadi mezani.
  Pamoja na dosari hizo za majaji, lakini shindano la Miss Tanga 2013 lililoandaliwa na Kampuni ya DATK Entertainment lilifana na Mkurugenzi wake, Asha Kigundula alitoa vyeti vya shukrani kwa watu na taasisi mbalimbali zilizomsaidia kufanikisha shughuli hiyo.
  Miongoni mwa waliopewa vyeti ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Hawa Dendegu, Ofisa Mtendaji Mkuu wa BIN ZUBEIRY Blog, Mahmoud Zubeiry na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba SC, Swedi Nkwabi. 
  Wasanii nyota Bi Hafua Suleiman, DK John wa lililokuwa kundi la Wagosi wa Kaya, Tunda Man wa Tip Top Connection walitumbuiza na kukonga nyoyo za mashabiki.
  Ni Tunda Man ndiye aliyesisimua zaidi kwa vibao vitamu, akisindikizwa na madansa wake waliopiga shoo kali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: LULU AMBONEA NDIYE MISS TANGA 2013, ILA MAJAJI... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top