• HABARI MPYA

  Alhamisi, Juni 20, 2013

  ARSENAL HUREEE, HIGUAIN TAYARI MGUU MMOJA LONDON

  IMEWEKWA JUNI 20, 2013 SAA 3:45 USIKU
  KLABU ya Arsenal imekubali kumpa mshahara wa Pauni 150,000 kwa wiki Gonzalo Higuain kuelekea usajili wa rejkodi wa klabu hiyo wa Pauni Milioni 22.
  kama BIN ZUBEIRY ilivyoandika mapema wiki hii, Arsenal imekubali kutoa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 22 kwa Real Madrid kwa ajili ya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25.
  Kiwango hicho kinavunja rekodi ya sasa ya klabu hiyo kununua mchezaji kwa bei kubwa, Pauni Milioni 15 ambazo ililipa kwa Zenit St Petersburg kumnunua Andrey Arshavin  Januari mwaka 2009. 
  On the move: How Higuain would look in an Arsenal kit, in our mocked-up image
  Anakuja: Jinsi Higuain atakavyoonekana katika jezi ya Arsenal

  Nyota huyo wa Real Madrid ameambiwa yuko huru kuondoka Bernebeu na Arsenal ipo karibu kabisa kumnasa mchezaji huyo ambaye imekuwa ikimmezea mate tangu akiwa River Plate, timu yake ya kwanza mwaka 2004.
  Arsenal ilijaribu kutaka kumsajili mshambuliaji huyo Muargentina mzaliwa wa Ufaransa mwaka 2006, lakini ikazidiwa kete na Real Madrid.
  Lakini Wenger sasa anakaribia kukata kiu yake ya kumsubiri kwa muda mrefu Higuain majira haya ya joto.
  Arsenal pia imeendelea na nia yake kutaka kuwasajili Wayne Rooney na Stevan Jovetic, lakini dili la Higuain linaonekana kuwa la ukweli zaidi.
  On the move: Real Madrid striker Gonzalo Higuain is closing in on a big-money switch to Arsenal
  Nyota wa Real Madrid, Gonzalo Higuain yupo karibu kutua Arsenal
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: ARSENAL HUREEE, HIGUAIN TAYARI MGUU MMOJA LONDON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top