• HABARI MPYA

  Ijumaa, Juni 21, 2013

  SIMBA SC YAMLIPA CHAKE BABU MFARANSA, KUONDOKA DAR WIKI IJAYO

  Amelipwa; Kocha Mfaransa wa Simba, Patrick Liewig akiwa na nahodha, Juma Kaseja. Amelipwa nusu, ataondoka na nyingine atalipwa Oktoba. 
  Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA JUNI 21, 2013 SAA 10:28 MCHANA
  KOCHA Mfaransa wa Simba SC, Patrick Liewig jana amelipwa dola za Kimarekani 10,000 kati ya dola 26,000 alizokuwa anadai klabu hiyo baada ya kumvunjia Mkataba na kiasi kilichobaki atalipwa Oktoba mwaka huu.
  Liewig alikuwa anadai malimbikizo ya mishahara ya miezi miwili, dola 12,000 na akalipwa dola 12,000 za kuvunjiwa Mkataba wakati dola 2,000 ni za tiketi yake ya kurejea kwake.
  Kocha huyo alivunjiwa Mkataba wakati amepwa likizo ya kwenda mapumzikoni kwao, baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na nafasi yake amepewa Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni’.
  Hata hivyo, baada ya kurejea nchini alifanya mazungumzo na uongozi wa Simba, hatimaye wamekubaliana kulipana kwa awamu, fungu la kwanza likitolewa jana.
  Sasa Liewig ataondoka Dar es Salaam wiki ijayo kurejea Ufaransa kusubiri malipo yake yaliyosalia. 
  Liewig alisani Mkataba wa mwaka mmoja na nusu Januari mwaka huu kuifundisha Simba SC akirithi mikona ya Mserbia, Profesa Milovan Cirkovick aliyetupiwa virago.     
  Katika kipindi chake cha kuwa na klabu hiyo kwa miezi mitano, Liewig aliiongoza Simba katika mechi 25 akiiwezesha kushinda tisa, sare nane na kufungwa saba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: SIMBA SC YAMLIPA CHAKE BABU MFARANSA, KUONDOKA DAR WIKI IJAYO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top