• HABARI MPYA

  Jumamosi, Juni 22, 2013

  TIOTE APANDISHWA KIZIMBANI ENGLAND KWA KUTUMIA LESENI FEKI YA UDEREVA

  IMEWEKWA JUNI 22, 2013 SAA 6:30 USIKU
  NYOTA wa Newcastle United, Cheick Tiote amepandishwa kizimbani kwa mashitaka matano, ikiwemo kutumia leseni feki ya udereva na kudanganya.
  Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ivory Coast, aliyetimiza miaka 27 jana, anatuhimiwa kutumia leseni feki ya udereva ya Ubelgiji na kufanya jithada za kupata leseni ya Uingereza.
  Tiote, aliyesajiliwa The Magpies kutoka FC Twente ya Uholanzi mwaka 2010, alisimamishwa na Polisi wa Northumbria karibu na Uwanja wa mazoezi wa klabu yake Februari 12 kwa kushukiwa kudanganya juu ya udereva wake.
  Cheick Tiote
  Kanjanja: Tiote, akiwasili mahakamani
  Cheick Tiote
  Mashitaka: Mchezaji wa Newcastle anakabiliwa na mashitaka matano

  Gari la kiungo huyo, aina ya Chevrolet Camaro, lenye thamani ya Pauni 75,000, lilifikishwa kituo cha Polisi  alipokamatwa.
  Tiote sasa atatakiwa kufika rufaa katika Mahakama Kuu ya Newcastle Julai 5.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: TIOTE APANDISHWA KIZIMBANI ENGLAND KWA KUTUMIA LESENI FEKI YA UDEREVA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top