• HABARI MPYA

    Monday, June 24, 2013

    NI HISPANIA NA ITALIA, URUGUAY NA BRAZIL NUSU FAINALI KOMBE LA MABARA...PATACHIMBIKA BABAKE!

    Fernando Torres amefunga tena leo

    IMEWEKWA JUNI 14, 2013 SAA 7:00 USIKU
    MABINGWA wa dunia, Hispania wametinga Nusu Fainali ya Kombe la Mabara kufuatia ushindi wa mabao wa 3-0 dhidi ya Nigeria usiku huu.
    Bao maridadi la juhudi binafsi za Jordi Alba, mmoja kati ya wachezaji wanane wa Barcelona kwenye kikosi cha kwanza cha Hispania, liliiweka Hispania mbele mbele baada ya dakika tatu, kabla ya Fernando Torres kufunga bao lake la tano kwenye mashindano haya dakika ya 62 kwa kichwa cha mkizi, dakika tatu tu aingine aingie kuchukua nafasi ya Roberto Soldado.
    Pamoja na kufungwa, Super Eagles walicheza vizuri na kilichowagharimu ni umaliziaji mbovu. Alba akafunga bao la tatu kwa Hispani na la pili kwake katika mchezo huo dakika ya 88.
    Matokeo hayo yanaifanya Hispania iongoze Kundi B kwa pointi zake tisa na itakutana na Italia waliowachapa 4-0 katika fainali ya mwaka jana ya Euro 2012 kwenye Nusu Fainali ya Kombe la Mabara Alhamisi mjini Fortaleza.
    Katika Nusu Fainali nyingine, Uruguay iliyoifunga 8-0 Tahiti usiku huu, imeshika nafasi ya pili kwenye Kundi hilo na itamenyana na Brazil katika Nusu Fainali. Nigeria baada ya kufungwa imemaliza katika nafasi ya tatu kwa pointi zake tatu ilizovuna kwa vibonde Tahiti.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: NI HISPANIA NA ITALIA, URUGUAY NA BRAZIL NUSU FAINALI KOMBE LA MABARA...PATACHIMBIKA BABAKE! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top