• HABARI MPYA

  Jumanne, Juni 25, 2013

  MMILIKI WA AC MILAN ATUPWA JELA MIAKA SABA KWA KUKUTWA NA HATIA YA KUFANYA NGONO NA KIBINTI CHA MOROCCO

  IMEWEKWA JUNI 25, 2013 SAA 9:00 USIKU
  MMILIKI wa AC Milan, Silvio Berlusconi amehukumiwa kifungo cha miaka saba jela na kufungiwa maisha kufanya kazi katika ofisi za umma baada ya kukutwa na hatia ya kumlipa binti mdogo afanye naye ngono katika moja ya pati zake za 'bunga bunga'.
  Waziri huyo Mkuu wa zamani wa Italia, Berlusconi, mwenye umri wa miaka 76, alimlipa binti mdogo wa Morocco, Karima El Mahroug, anayekwenda kwa jina la utani, Ruby, kwa ajili ya ngono na baadaye akajaribu kumbambikizia kesi ya wizi kwa kuwapigia simu Polisi na binti huyo akakamatwa. Berlusconi na mwanamke huyo wamekanusha kufanya ngono.
  Mwendesha mashitaka alipendekeza afungwe miaka sita kwa kuzini ni binti mdogo na matumizi ya nguvu, lakini majaji watatu wa kike katika Mahakama ya Jijini Milan jana walitaka afungwe muda mrefu zaidi, miaka saba. 
  Verdict: Italy's former Prime Minister Silvio Berlusconi, pictured last year, was found guilty today of paying Moroccan Karima El Mahroug, nicknamed Ruby the Heart-stealer, for sex at a 'bunga bunga' party
  Verdict: Italy's former Prime Minister Silvio Berlusconi, pictured last year, was found guilty today of paying Moroccan Karima El Mahroug, nicknamed Ruby the Heart-stealer, for sex at a 'bunga bunga' party
  Mfungwa: Mmiliki wa AC Milan, Silvio Berlusconi (kushoto) amekutwa na hatia ya kumlipa binti mdogo wa Morocco, Karima El Mahroug wafanye naye ngono
  San Siro: Berlusconi is the owner of AC Milan, pictured here with former maanger Carlo Ancelotti in 2007
  San Siro: Berlusconi ni mmiliki wa AC Milan, hapa akiwa katika picha ya pamoja na kocha wa zamani wa klabu hiyo, Carlo Ancelotti mwaka 2007

  Berlusconi pia amefungiwa maisha kufanya kazi katika ofisi za umma baada ya Waziri huyo Mkuu wa zamani kukutwa na hatia leo. 
  Lakini mfungwa huyo anaweza kukata rufaa mara mbili kabla hajamaliza kifungo chake, ambayo inaweza kuchukua miezi au miaka.
  Maana yake hatatumikia kifungo chake hadi ashindwe rufaa zake. 
  Klabu yake ya AC Milan - ambayo amekuwa Rais wake kwa vipindi vitatu tofauti tangu mwaka 1987 - inayoundwa na nyota kadhaa akiwemo Mario Balotelli - ilimaliza katika nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu ya Italia, Serie A msimu uliopita ikizidiwa pointi 15 nyuma ya wapinzani, Juventus.
  Sentenced: President of the court Giulia Turri (centre) read out the damning verdict
  Kifungo: Rais wa Mahakama, Giulia Turri (katikati) akisoma hukumu

  Baada ya hukumu, Mwanasheria wa Berlusconi, Niccolo Ghedini, mara moja alitangaza kukata rufaa akisema hukumu hiyo ni kama ilivyotarajiwa, haikutenda haki.
  "Hii ni kinyume cha uhalisia," Ghedini aliwaambia Waandishi wa Habari nje ya Mahakama. "Nimetulia kwa sababu nimekuwa nikisema kwa miaka mitatu kwamba kesi haiwezi kuendeshwa hapa," alisema Ghedini. 
  Alias: Karima el-Mahroug is better known as 'Ruby the Heartbreaker'
  Kimwana: Karima el-Mahroug anafahamika kama 'Ruby the Heartbreaker'
  Alisema pati hiyo ya chakula cha usiku ilikuwa kwa ajili ya watu maaum; Mwendesha mashitaka amesema walifanya ngono na mwanamke huyo aliyelipwa kuhudhuria.
  Hata kama Berlusconi alikuwa anamjua mwanamke huyo katikati ya kesi hiyo, Karima el-Mahroug, anafahamika vyema kwa jina lake la utani, Ruby the Heart Breaker, ametoa ushahidi.
  Alikuwa ana umri wa miaka 17 wakati huo anadaiwa kufanya kitendo hicho, lakini sasa amefikisha miaka 24. wakati umri wa kufanya ngono Italia ni miaka 14, na ni kinyume cha sheria kumlipa binti aliye chini ya umri wa miaka 18 kwa ajili ya ngono.
  El-Mahroug aliitwa kwa utetezi, lakini akashindwa kutokea kwa sababu kadhaa,kuchelewesha hukumu. Timu ya Berlusconi mara moja ikamengua katika orodha ya mashahidi.
  Statement: Silvio Berlusconi's lawyer Niccolo Ghedini speaks to reporters outside the courthouse in Milan, Italy, today after judges found him guilty of having sex with a minor
  Maelezo: Mwanasheria wa Silvio Berlusconi, Niccolo Ghedini akizungumza na Waandishi wa Habari nje ya Mahakama jana Jijini Milan, Italia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: MMILIKI WA AC MILAN ATUPWA JELA MIAKA SABA KWA KUKUTWA NA HATIA YA KUFANYA NGONO NA KIBINTI CHA MOROCCO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top