• HABARI MPYA

    Tuesday, June 18, 2013

    ARSENAL KUMALIZANA NA HIGUAIN WIKI HII, KUSAJILI PIA KINDA LA U-21 YA HISPANIA LINALOITOA UDENDA NA REAL MADRID

    IMEWEKWA JUNI 18, 2013 SAA 2:00 ASUBUHI
    KLABU ya Arsenal inatumai kumaliza miaka tisa ya kusubiri saini ya Gonzalo Higuain wiki hii kwa kuweka rekodi ya dau lake la usajili, Pauni Milioni 22 ofa waliyotoa kumnasa mshambuliaji huyo.
    BIN ZUBEIRY inafahamu Muargentina huyo amekubali kuhamia Emirates majira haya ya joto na The Gunners - ambao pia wanaamini watambakiza beki Bacary Sagna na Laurent Koscielny kuelekea msimu ujao - wiki hii itafanya mipango rasmi ya kumsaini nyota huyo wa Real Madrid, ambaye ameambiwa yuko huru kuondoka Bernebeu.
    On target: Real Madrid striker Gonzalo Higuain could become Arsenal's record signing in a £22m deal
    Anatakiwa: Mshambuliaji wa Real Madrid, Gonzalo Higuain anaweza kuibuka mchezaji ghali kuwahia kusajiliwa Arsenal, kwa Pauni Milioni 22
    Watchful eyes: Arsenal boss Arsene Wenger has been reluctant to splash out hefty fees for players in the past
    Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger yuko tayari kumwaga fedha kusajili

    Mazungumzo baina ya viongozi wa Arsenal na wawakilishi wa Higuain yanaendelea vizuri na inasemekana kilichobaki ni klabu hizo mbili kukubaliana.
    Kwa sasa dau kubwa la usajili walilowahi kutoa ni Pauni Milioni 15 kwa Zenit St Petersburg kumsajili Andrey Arshavin, Arsenal iko tayari kumpa mshahara wa Pauni 150,000 kwa wiki Higuain.
    The Gunners imekuwa ikimmezea mate mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 tangu akiwa River Plate, timu yake ya kwanza mwaka 2004.
    Flop: The disappointing £15m capture of Andrey Arshavin is Arsenal's current record transfer fee
    Amechuja: Andrey Arshavin amechemsha Arsenal licha ya kushikilia rekodi ya kusajiliwa bei mbaya

    Arsenal ilijaribu uwezekano wa kumsajili Muargentina huyo mzaliwa wa Ufaransa mwaka 2006, lakini wakazidiwa kete na Real Madrid.
    Lakini Wenger anatarajiwa kukata kiu yake ya muda mrefu kwa mshambuliaji huyo, Higuain hivi karibuni.
    Arsenal imeendelea na nia yake thabiti ya kutaka kuwasajili  Wayne Rooney na Stevan Jovetic, lakini dili la Higuain ndilo la ukweli zaidi.
    Young Gun? Arsenal are also lining up a move for Spanish U21 star Asier Illarramendi (centre)
    Mtutu mdogo? Arsenal pia inataka kumsajili mchezaji wa U21 ya Hispania, Asier Illarramendi (katikati)

    Wakati huo huo, The Gunners wanaongoza mbio ya kuwania saini ya nyota wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 21 ya Hispania, Asier Illarramendi. 
    Kiungo huyo wa ulinzi wa Real Sociedad mwenye thamani ya Pauni Milioni 10 anang'ara kwa sasa na anaitoa udenda na Real Madrid pia. 
    Arsenal pia inamfuatilia Gilbert Imbula - lakini Illaramendi akuwa sahihi zaidi akicheza na Mikel Arteta.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: ARSENAL KUMALIZANA NA HIGUAIN WIKI HII, KUSAJILI PIA KINDA LA U-21 YA HISPANIA LINALOITOA UDENDA NA REAL MADRID Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top