• HABARI MPYA

  Jumatano, Juni 26, 2013

  CAVANNI AWAKARIPIA WAZAZI WAKE..."ACHENI KUNIZUNGUMZIA KATIKA UMMA"

  IMEWEKWA JUNI 26, 2013 SAA 12:30 ASUBUHI
  MSHAMBULIAJI wa Napoli, Edinson Cavani amewapiga stop wazazi wake kuzungumzia mustakabali wake kwenye umma.
  Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 wa Uruguay, alikuwa tayari amehusishwa na mpango wa kuhamia Manchester City, kabla ya mama yake kusema amefanya mazungumzo na klabu zote, City na Real Madrid.
  Kisha maelezo ya baba yake yakapendekeza Cavani amekubali kujiunga na Real, kwa dau la Euro Milioni 63 (Pauni Milioni 54).
  Hitting out: Cavani trains with his Uruguay team-mates in Brazil on Tuesday
  Amewatolea uvivu: Cavani akifanya mazoezi na wachezaji wenzake wa Uruguay nchini Brazil jana
  Hitting out: Cavani trains with his Uruguay team-mates in Brazil on Tuesday
  Lakini Cavani, ambaye amefunga mabao 29 katika ligi akiwa na Napoli msimu uliopita, amewataka wazazi wake wakae kimya na wakati ukifika utatoa majibu.
  Akinukuliwa na La Repubblica, aliwaambia Waandishi wa Habari: "Baba yangu amezungumza kuhusu Real? Nataka niseme hayo maneno si yangu.
  "Nimewaambia wazazi wangu mara elfu, wasizungumze tena. Wanaweza kuniumiza tu mimi.
  "Mimi ni mali ya Napoli kama ilivyo na hiyo itategemea na klabu. Kama suluhisho lingine, litakuja lenyewe, tutamua.'
  Wanted man: Cavani is one of Europe's hottest properties
  Lulu: Cavani ni mmoja wa wachezaji adimu Ulaya
  Rais wa Napoli, Aurelio De Laurentiis ameripotiwa akisema mshambuliaji wake huyo anatakiwa kufanya uamuzi juu ya mustakabali wake hadi kufikia Julai 20, akirejea kutoka kwenye Kombe la Mabara anakoiwakilisha Uruguay.
  Na alipoulizwa ikiwa Real Madrid - ambayo sasa iko chini ya kocha wa zamani wa Chelsea na Paris Saint-Germain, Carlo Ancelotti - itakuwa sehemu yake sahihi, Cavani alibakia kuficha.
  "Nitaweka wazi juu ya hilo pia - wakati wote nimekuwa nikisema ni moja ya klabu bora duniani.
  Prolific: The Uruguayan was top scorer in Serie A last season
  Anatisha: Nyota huyo wa Uruguay amekuwa mfungaji bora wa Serie A msimu uliopita
  "Wote tumekuwa tukiota vizuri tu kuchezea timu yao, kama ambavyo tunaota kuhusu Barcelona, lakini sasa nipo Napoli na ninajivunia kwa kweli.
  "Kama nitaiacha nyuma jezi ya bluu siku moja, nitajiunga na klabu kubwa tu. Wazi kuna mashabiki ambao wataelewa na wengine ambao hawataelewa.
  "Lakini sitaki kuteleza nyuma ya mlango, Nataka kutoka mbele ya mlango, siku ambayo hatimaye mambo yatakuwa,".
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: CAVANNI AWAKARIPIA WAZAZI WAKE..."ACHENI KUNIZUNGUMZIA KATIKA UMMA" Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top