• HABARI MPYA

  Jumapili, Juni 30, 2013

  PELLE ATAMBULISHWA MAN CITY..HIYO MIKOGO YAKE MBONA MANCHESTER PATACHIMBIKA

  IMEWEKWA JUNI 30, 2013 SAA 4:00 USIKU
  KOCHA mpya wa Manchester City, Manuel Pellegrini amewasili England tayari kurithi rasmi mikoba ya Roberto Mancini Uwanja wa Etihad.
  Raia huyo wa Chile alitumia muda fulani kushangaa shangaa maeneo ya Jiji la Manchester na kuchukua suti iliyo sawa yake katika duka la Hugo Boss kabla ya kutambulishwa na kukabidhiwa jezi ya bluu.
  Alikuwa na wasaidizi wake akiwemo Ruben Cousillas na kocha wa ufiti, Jose Cabello.
  Touchdown in England: Manuel Pellegrini showing off the Manchester City shirt for the first time
  Ametua England: Manuel Pellegrini akionyesha jezi ya Manchester City kwa mara ya kwanza
  New horizons: Pellegrini arriving at Manchester Airport with some of his backroom staff
  Pellegrini akiwasili Uwanja wa Ndege wa Manchester na wasaidizi wake
  Calling a cab: Pellegrini getting around Manchester using his good English
  Akiita teksi: Pellegrini katika jiji la Manchester akizungumza kiingereza kizuri

  Mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 59, amejiunga na timu hiyo kutoka Malaga, na anatakiwa haraka kuhakikisha timu inafanya vizuri ili kuwafurahisha mashabiki na watu wa klabu hiyo.
  Mpinzani wake mpya Manchester, David Moyes, anaanza kazi kesho United na Pellegrini atatazamiwa kumpiga bao kuanzia katika usajili.
  City tayari imepigwa bao na Real Madrid katika saini ya kijana wa zamani wa Pellegrini, Isco, ambaye aling'ara katika Kombe la Euro kwa vijana chini ya umri wa miaka 21 nchini Israel akiwa na Hispania iliyotwaa ubingwa.
  First greetings: Pellegrini meeting a delegation from Manchester City in the early hours of Sunday morning
  Salamu ya kwanza: Pellegrini alikutana na msafara kutoka Manchester City katika saa zake za mwanzoni asubuhi
  Suits you! It appears City will lose none of Mancini's taste in nice outfits
  Suti yako! akiangalia suti
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: PELLE ATAMBULISHWA MAN CITY..HIYO MIKOGO YAKE MBONA MANCHESTER PATACHIMBIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top