• HABARI MPYA

  Jumatano, Juni 19, 2013

  AVB AWAPIGA CHINI PSG, WAANGUKIA KWA CAPELLO

  IMEWEKWA JUNI 19, SAA 1:30 ASUBUHI 
  KOCHA Andre Villas-Boas ameripotiwa kupiga chini ofa ya kuifundisha Paris Saint-Germain ili abaki Tottenham.
  Mabingwa hao wa Ufaransa walitaka Mreno huyo arithi mikoba ya Carlo Ancelotti, anayeelekea Real Madrid, lakini sasa wamehamishia mawindo yao kwa Fabio Capello.
  Inafahamika Villas-Boas alipewa ofa ya Mkataba wa miaka mitatu na mabilionea wa Qatari wanaoimiliki PSG baada ya majadiliano na wakala wake, Carlos Goncalves, lakini mwalimu huyo kijana wa miaka 35 anataka kufanya mambo adimu Spurs waliomchukua msimu uliopita baada ya kutupiwa virago Chelsea.
  Staying put: Villas-Boas is reportedly looking to stay at White Hart Lane
  Anabakit: Villas-Boas ameripotiwa kubaki White Hart Lane
  Work to do: Villas-Boas will be looking to take Spurs up a notch after their fifth-place finish last season
  Kazi ya kufanya: Villas-Boas anataka kuipaisha matawi ya juu zaidi Spurs kutoka nafasi ya tano aliyowapa msimu uliopita

  Tottenham wanatarajiwa kubomoa benki kumpa fedha za kutosha Villas-Boas, aliyebakiza miaka miwili katika Mkataba wake White Hart Lane, ili kujenga kikosi cha nguvu cha kukata tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa.
  Miongoni mwa wachezaji anaowataka ni kiungo wa Corinthians, Paulinho, wakati Spurs pia ni klabu pekee iliyoomba kumsajili kiungo wa Atletico Mineiro, Bernard. Wakala wake amesema: "Dortmund hawajawasilisha mapendekezo na Tottenham ni washindani pekee,".
  Villas-Boas pia inaelezwa anavutiwa na ushindani wa kupambana na bosi wake wa zamani, Mreno mwenzake Jose Mourinho katika Ligi Kuu England msimu ujao.
  Plan B: Russia boss Capello could be drafted in for a season
  Mpango B: Kocha wa Urusi, Capello anaweza kuwa kazini msimu ujao

  Taarifa za jana usiku nchini Ufaransa zinasema kocha wa zamani wa England, Capello atakuwa mwalimu mpya wa PSG kwa Mkataba wa mwaka mmoja.
  Kocha wa zamani wa England, Capello anatazamiwa kuwa mpango B wa PSG, licha ya kwamba bado ana Mkataba wa mwaka mmoja Urusi.
  Urusi ipo kwenye nafasi nzuri ya kufuzu kwenye Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil,na kuna uwezekano Capello akarejea katika timu hiyo ya taifa baada ya msimu mmoja na PSG kukamilisha majukumu yake katika Kombe la Dunia.
  Merry-go-round: Carlo Ancelotti looks to be on his way to Real Madrid
  Carlo Ancelotti anatarajia kuhamia Real Madrid
  Big season: PSG were French champions, and are looking to build an empire
  Msimu mzuri: PSG walikuwa mabingwa Ufaransa na wanataka kujiimarisha zaidi
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: AVB AWAPIGA CHINI PSG, WAANGUKIA KWA CAPELLO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top