• HABARI MPYA

  Jumanne, Juni 18, 2013

  'WALLAHI' AVB KAWASHIKA PABAYA SPURS...NA HATA REAL WAMUONA BONGE LA 'MCHAWI'

  IMEWEKWA JUNI 18, 2013 SAA 8:40 MCHANA
  KOCHA Andre Villas-Boas atataka uhakika juu ya Tottenham kumbakiza Gareth Bale na kupewa fungu la kusajili wachezaji anaowataka kabla ya kujifunga katika klabu hiyo.
  Kama ambavyo BIN ZUBEIRY iliripoti wiki iliyopita, Mreno huyo anatakiwa na Paris Saint-Germain akachukue nafasi ya mwalimu anayehamia Real Madrid, Carlo Ancelotti.
  Mwenyekiti wa Tottenham, Daniel Levy anataka kumbakiza kocha wake huyo wa thamani ya juu White Hart Lane msimu ujao.
  Crunch time: Andre Villas-Boas wants Tottenham to ensure Gareth Bale stays at the north-London club
  Andre Villas-Boas anataka Tottenham imuhakikishie Gareth Bale atabaki Kaskazini mwa London

  Lakini Spurs wanafahamu Villas-Boas akienda PSG lazima kocha huyo wa zamani wa Chelsea agharimiwe Pauni Milioni 10 za kuvunja Mkataba.
  Wakuu wa Tottenham wanaamini mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 35 anataka kubaki na kukamilisha kazi yake aliyoianza Spurs.
  Lakini inafahamika AVB yuko katika nafasi ya kutumia kuhitajiwa kwake na PSG kuushinikiza uongozi utimize matakwa yake majira haya ya joto.
  Kuhakikishiwa kubaki kwa Bale, anayetakiwa na PSG na Real Madrid, ndio kipaumbele cha Villas-Boas kipindi hiki, lakini pia anataka kuboresha safu yake ya ushambuliaji.
  Crucial: Whether star man Gareth Bale leaves the club could prove decisive in Villas-Boas' future
  Hatari: Aidha nyota Gareth Bale abaki ili Villas-Boas abaki, au waondoke wote.

  David Villa na Roberto Soldado wote wanahitajiwa, wakati Spurs inammezea mate kwa muda mrefu Leandro Damiao.
  And Villas-Boas anataka kuhakikishiwa Levy anafanya jitihada za kuhakikisha anakamilisha mapendekezo yake kabla hajaamua mustakabali wake.
  David Villa
  Leandro Damiao
  Walengwa wakuu: Leandro Damiao (kulia) na mshambuliaji wa Barcelona, David Villa (kushoto) wote wanatakiwa
  Killer touch: Roberto Soldado netted during Spain's Confederations Cup victory over Uruguay
  Roberto Soldado aliifungia Hispania katika Kombe la Mabara dhidi ya Uruguay
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: 'WALLAHI' AVB KAWASHIKA PABAYA SPURS...NA HATA REAL WAMUONA BONGE LA 'MCHAWI' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top