• HABARI MPYA

  Jumamosi, Juni 29, 2013

  TWANGA PEPETA KUZINDUA ALBAMU YAKE YA 12 LEADERS CLUB KESHO

  Wanamuziki wa Twanga Pepeta
  Na Majuto Omary, IMEWEKWA JUNI 29, 2013 SAA 7:44 MCHANA
  BENDI ya African Stars “Wana Twanga Pepeta”  kesho Jumapili itazindua albamu yake 12 ijulikanyo kwa jina la Nyumbani Ni Nyumbani kwenye viwanja vya Leaders Club huku ikisherehekea miaka 15 tokea kuanzishwa kwake.
  Uzinduzi huo utapambwa  na michezo mbali mbali kuanzia saa 3.00 asubuhi ambapo timu nane za mpira wa miguu zitawania zawadi mbali mbali katikamichuano ijulikanalo kwa jina la ASET Bonanza. Timu hizo zitaongozwa na ile ya waandishi wa habari za michezo, Taswa FC na nyingine kama Brake Point, Mango, Namanga, Kivukoni, Camp Combine, Wagadau na Kunduchi.
  Mbali a burudani kutoka kwa Twanga Pepeta, siku hiyo pia kutakuwa na burudani kutoka kwa wanamuziki wa kizazi kipya, Linex, Barnaba, bila kusahau, wakongwe wa muziki wa dansi nchini, bendi ya Mlimani Park maarufu kwa mtindo wa Sikinde Ngoma ya Ukae.
  Mkurugenzi wa kampuni ya ASET inayomili bendi hiyo, Asha Baraka alisema kuwa bendi inayoundwa na wanamuziki chipukizi au Yosso, Aset Academia nayo itatoa burudani ya utangulizi katika uzinduzi huo uliodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro, Clouds Media Group, Radio One na CXC Africa.
  Asha alisema kuwa wamejipanga kukoga nyoyo za mashabiki siku hiyo kwani wameandaa shoo mbali mbali zijulikanazo kwa jina la Twanga 2013 na nyimbo zao mpya zilizomo kwenye albamu hiyo ambazo ni Nyumbani ni Nyumbani uliyotungwa na Kalala Junior, Ngumu Kumeza (Ibrahim Mpoyo), Mwenda Pole (Badi Bakule), Kila Nifanyalo (Jumanne Saidi), Shamba la Twanga (Greyson Semsekwa na Twanga 2013 ambao ni utunzi wa wanamuziki wote wa bendi hiyo.
  Albamu nyingine za bendi hiyo ni Kisa Cha Mpemba iliyozinduliwa mwaka 1999, Jirani (2000), Fainali Uzeeni (2001),  Chuki  Binafsi (2002), Ukubwa Jiwe (2003), Mtu Pesa (2004), Safari (2005),Password (2006),  Mtaa wa Kwanza (2007),  Mwana Dar es Salaam (2009) na Dunia Daraja iliyozinduliwa mwaka 2011.
  Asha alisema kuwa wameamua kufanya hivyo ili kuwakumbusha mashabiki wao wapi walipoanzia (tokea) na wapi wanapokwenda katika muziki wa dansi. Alisema kuwa kimuziki wamepata mafanikio makubwa sana kutokana na kupata mialiko ya kimataifa kama nchi za Ulaya mama Uingereza, Ujerumani, Uholanzi, Finland, Norway na nyingine nyingi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: TWANGA PEPETA KUZINDUA ALBAMU YAKE YA 12 LEADERS CLUB KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top