• HABARI MPYA

    Friday, April 20, 2012

    WASWAZI KUCHEZESHA SIMBA NA AL AHLY SHANDY


    Simba SC

    SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Swaziland kuchezesha mechi ya kwanza ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho kati ya Simba na Al Ahly Shandy ya Sudan itakayochezwa Aprili 29 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Waamuzi hao wa mechi hiyo namba 71 ni Nhleko Simanga Pritchard atakayepuliza filimbi wakati wasaidizi wake ni Mbingo Petros Mzikayifani na Sibandze Thulani. Mwamuzi wa mezani atakuwa Fakudze Mbongiseni Elliot.
    CAF pia imemteua Kayijuga Gaspard wa Rwanda kuwa Kamishna wa mechi hiyo.
    Wakati huo huo: Kampuni nne kati ya sita zimepita hatua ya kwanza ya mchakato wa kupata moja itakayofanya kazi ya kutengeneza tiketi za elektroniki kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu ya Vodacom na nyingine zinazosimamiwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
    Shughuli ya ufunguzi wa maombi ya hatua ya awali ya kuonesha nia (Expression of Interest) kwa ajili ya tenda hiyo ilifanywa jana (Aprili 19 mwaka huu) na Kamati ya Mipango na Fedha ya TFF ambayo ndiyo Bodi ya Tenda ya shirikisho.
    Kampuni ambazo zimepita hatua hiyo ya kwanza sasa zinatakiwa kuwasilisha rasmi tenda zao kwa ajili ya shughuli hiyo ndani ya kipindi cha wiki tatu tangu ulipofanyika ufunguzi wa hatua ya kwanza.
    Baadaye Bodi ya Tenda itakutana tena kupitia tenda zitakazokuwa zimewasilishwa na kufanya uteuzi wa kampuni moja itakayofanya kazi hiyo.
    Kampuni ambazo zimefanikiwa kuingia katika hatua hiyo ya pili ni CRDB Bank PLC, SKIDATA People Access Inc., Prime Time Promotions na Punchlines (T) Limited.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WASWAZI KUCHEZESHA SIMBA NA AL AHLY SHANDY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top