| Thomas Ulimwengu, tegemeo la Ngorongoro |
SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limewateua waamuzi kutoka
Uganda, nchi anayotoka mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi kuchezesha mechi ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya
miaka 20 kati ya Tanzania (Ngorongoro Heroes) na Sudan itakayofanyika Aprili 21
mwaka huu.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace
Wambura ameiambia bongostaz.blogspot.com mchana huu kwamba refa atakayechezesha
mechi hiyo itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili
jioni ni Brian Miiro.Wambura amesema Waamuzi wasaidizi ni Mark Ssonko na Lee Patabali wakati mwamuzi wa mezani ni Denis Batte.
Ejigu Ashenafi wa Ethiopia ndiye ameteuliwa kuwa Kamisaa wa mechi hiyo namba 15.
Kamisaa na waamuzi hao watawasili nchini Aprili 19 mwaka huu kwa ndege za Ethiopian Airlines na Air Uganda.


.png)
0 comments:
Post a Comment