• HABARI MPYA

    Tuesday, April 17, 2012

    SIMBA TAIFA, YANGA KAITABA KESHO

    Vinara wa Ligi Kuu, Simba ambao kesho watakuwa wenyeji wa JKT
    LIGI Kuu Vodacom Tanzania Bara, kinaendelea tena kesho (Aprili 18 mwaka huu) kwa mechi tano zitakazochezwa kwenye miji ya Bukoba, Mwanza, Dar es Salaam, Mlandizi na Dodoma.
    Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace Wambura ameiambia bongostaz.blogspot.com mchana huu kwamba mabingwa watetezi Yanga watakuwa wageni wa Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba wakati Toto Africans itaikaribisha African Lyon kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
    Wambura amesema vinara wa ligi hiyo Simba wataoneshana kazi na JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Ruvu Shooting na Moro United zitaumana kwenye Uwanja wa Mabatini mjini Mlandizi.
    Nayo Polisi Dodoma itakuwa mwenyeji wa Coastal Union mjini Dodoma.
    Wakati huo huo: Wambura amesema Sekretarieti ya TFF kesho (Aprili 18 mwaka huu) itafungua maombi ya tenda zilizowasilishwa na kampuni mbalimbali kwa ajili ya kutengeneza tiketi za elektroniki.
    Maombi hayo yatafunguliwa saa 9 alasiri kwenye ofisi za TFF ambapo kampuni zote zilizowasilisha tenda zinatakiwa kuwepo wakati wa ufunguzi huo.
    Machi 9 mwaka huu TFF ilitangaza tenda kwa ajili ya kutengeneza tiketi za elektroniki kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu ya Vodacom na mechi nyingine inazozisimamia.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA TAIFA, YANGA KAITABA KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top