• HABARI MPYA

    Thursday, August 17, 2017

    NYOTA WATATU SERENGETI BOYS WAENDA ETOILE DU SAHEL TUNISA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    WACHEZAJI watatu waliokuwa kwenye timu ya soka ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys, Ally Ng’anzi, Yohana Oscar Nkomola na Erick Nkosi wameondoka nchini Alfajiri ya leo kwenda Tunisia kwa ajili ya majaribio ya kucheza soka ya kulipwa.
    Serengeti Boys ikiundwa na vijana wenye vipaji kutoka mikoa tofauti, iliweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza ya vijana Tanzania kucheza Fainali za Afrika baada ya kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 mwezi Mei mwaka huu nchini Gabon. 
    Nyota wa Serengeti Boys, Ally Ng’anzi, Yohana Oscar Nkomola na Erick Nkosi wakiwa na Mtendaji Mkuu w Cambiasso, Twaha Ngwambia

    Na kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu wa Cambiasso Sports Centre, Twaha Ngwambi, vijana hao wote wamepata mwaliko wa klabu ya Etoile du Sahel ya Ligi Kuu ya Tunisia.
    Ngwambia amesema mwaliko huo unafuatia vijana hao wote kufanya vizuri wakiwa na timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 mwaka huu.
    “Na hii klabu ilivutiwa na hawa vijana baada ya mechi za awali tu za Serengeti Boys kabla hata uya kwenda Fainali za Gabon, lakini ilishindikana kwenda mapema kwa sababu ya maandalizi ya fainali za Gabon kwa sababu walikwedna kuweka kambi Moroccomwezi mzima,”amesema. 
    Ngwambia amesema kwamba Ng’anzi na Nkosi wanakwenda kufanya majaribio, wakati Nkomola anakwenda moja kwa moja kujiunga na akademy ya timu hiyo ambako atasaini mkataba.
    Pamoja na kutolewa katika hatua ya makundi nchini Gabon, Serengeti Boys ilivutia kwa soka yake, huku vijana wengi wakitabiriwa kufika mbali zaidi kisoka.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NYOTA WATATU SERENGETI BOYS WAENDA ETOILE DU SAHEL TUNISA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top