• HABARI MPYA

  Monday, August 21, 2017

  NEYMAR APIGA MBILI PSG 'IKIFUNGULIA MBWA' LIGUE 1, YAUA 6-2

  Neymar akikimbia baada ya kuifungia bao la kwanza Paris Saint Germain dakika ya 31 kati ya mawili, lingine dakika ya 90 na ushei usiku wa Jumapili katika ushindi wa 6-2 dhidi ya Toulouse kwenye mchezo Ligue 1, Ufaransa Uwanja wa Parc des Princes. Mabao mengine ya PSG yamefungwa na Adrien Rabiot dakika ya 35, Edinson Cavani dakika ya 75,  Javier Pastore dakika ya 82 na Layvin Kurzawa dakika ya 84 wakati ya Toulouse iliyomaliza pungufu kufuatia kiungo wake Mtaliano, Marco Verratti kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 69 baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano yalifungwa na Max Gradel dakika ya 18 na Thiago Silva aliyejifunga dakika ya 78 PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NEYMAR APIGA MBILI PSG 'IKIFUNGULIA MBWA' LIGUE 1, YAUA 6-2 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top