• HABARI MPYA

  Thursday, August 31, 2017

  ‘DIMBA MUSIC CONCERT KIVUMBI’ SI YA KUKOSA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MAANDALIZI ya Tamasha kubwa la muziki wa Dansi lijulikano kama 'Dimba Music Concert Kivumbi' litakalojumuisha pambano kati ya Msondo Ngoma na  timu ya Taifa ya Dansi litakolanyika Septemba 2 yamekamilika.
  Tamasha hilo litafanyika katika ukumbi wa Travertine Magomeni kuanzia saa 2 usiku ambapo timu ya taifa ya Dansi itaongozwa na Juma Kakere, Hussein Jumbe, Mwinjuma Muumin, Ally Choki na Nyoshi El Saadat ambao wametunga nyimbo 10 mpya kwa ajili shughuli hiyo.
  Mwenyekiti wa kamati wa ya maandalizi ya Tamasha hilo Jim Chika amesema kwa miaka 20 sasa gazeti la Dimba limekuwa likisapoti muziki wa Dansi kwa kuandika lakini wameanza kuandaa matamasha kuendelea kuunga mkono ili kuufikisha mbali.
  Wanamuziki maarufu, Mwinjuma Muumini 'Kocha wa Dunia' (kulia) na Ally Choky (kushoto) watakuwepo

  Mratibu wa Tamasha, Mwani Nyangassa (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari leo
  "Tumekuwa tukiandika stori kuhusu muziki wa Dansi kwa miaka 20, sasa tumeanza kuandaa matamasha na Jumamosi tutakuwa ukumbi wa Travertine katika pambano kati ya Msondo Ngoma na timu ya Taifa ya Dansi," alisema Chika.
  Kwa upande wa Muumin amewataka wadau wa muziki wa Dansi kujitokeza kwa wingi kwakua kutakuwa na 'suprize' ya nyimbo mpya huku pia akiahidi  nyimbo ya 'kikombe kimoja' siku hiyo.
  Nae El Saadat 'Rais wa vijana' amesema muziki wa dansi haujafa kama watu wanavyodhani na kulithibitisha hilo Jumamosi watashusha burudani ya kutosha.
  Kiingilio katika Tamasha hilo VIP itakuwa sh 20,000 kawaida sh 10,000.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ‘DIMBA MUSIC CONCERT KIVUMBI’ SI YA KUKOSA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top