• HABARI MPYA

  Tuesday, August 29, 2017

  SANGA WA YANGA AWANIA UENYEKITI BODI YA LIGI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KAMATI ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imetangaza majina nane ya wagombea ambao yamepita katika mchujo wa awali kuwania nafasi mbalimbali katika Kamati ya Uongozi (Management Committee) ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
  Waliopitishwa ni kuwania Uenyekiti wa Kamati ya Uongozi ni Kaimu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga na Ahmed Yahya wa Kagera Sugar wakati Shani Chrisostoms  ameiptishwa kuwania nafasi ya Makamu mwenyekiti. 
  Kwa mujibu wa kamati hiyo, Ramadhan Mahano na Hamisi Madaki wamepitishwa kuwania nafasi ya Ujumbe wakitokea klabu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Clement Sanga (kushoto) akiwa na aliyekuwa Mwenyekiti wake, Yussuf Manji
  James Bwire na Almas Kasongo wamepitishwa kuwania Ujumbe wakitokea klabu za Ligi Daraja la Kwanza. Brown Ernest hakupitishwa kwa sababu hakuthibitishwa na klabu yake. Edga Chubura amepitishwa kuwania ujumbe akitokea klabu za Ligi Ligi Daraja la Pili.
  Wagombea kwa mujibu wa kanuni za uendeshaji wa Bodi ya Ligi Kuu ni marais au wenyeviti wa klabu husika. Wagombea wanatakiwa kuwa wenyeviti au Marais wa klabu husika. Nafasi ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania inagombewa na klabu za Ligi Kuu pekee.
  Uchaguzi huo wa kamati hiyo utafanyika Jumapili Oktoba 15, 2017 jijini Dar es Salaam na unaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za Uchaguzi za TFF toleo la 2013.
  Wakati huo huo: Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limetoa Ngao ya Jamii mpya kwa ajili ya kuipa Simba ambayo ilifanikiwa kuishinda Young Africans katika mchezo kuwania taji hilo uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Agosti 23, mwka huu.
  Siku hiyo mara baada ya mchezo ambao Simba ilishinda kwa mikwaju ya penalti 5-4, TFF ilitoa Ngao ya Jamii ambayo ilikuwa na makosa ya maandishi yaliyoonekana kwenye hivyo kuzua taharuki kwa wanafamilia wa mpira wa miguu.
  TFF iliomba radhi na kuahidi kutoa Ngao ya Jamii nyingine ambayo sasa imetolewa leo Jumanne Agosti 29, mwaka huu na itakabidhiwa kwa Simba kabla ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom  dhidi ya Azam FC jijini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SANGA WA YANGA AWANIA UENYEKITI BODI YA LIGI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top