• HABARI MPYA

  Friday, August 25, 2017

  ARSENAL YAPANGWA NA FC COLOGNE, BATE LIGI YA ULAYA

  MAKUNDI YOTE LIGI YA ULAYA:
  KUNDI A: Villarreal (Hispania), Maccabi Tel-Aviv (Israel), Astana (Kazakhstan), Slavia Praha (Jamhuri ya Czech)
  KUNDI B: Dynamo Kyiv (Ukraine), Young Boys (Uswisi), Partizan (Serbia), Skenderbeu (Albania)
  KUNDI C: Sporting Braga (Ureno), Ludogorets (Bulgaria), Hoffenheim (Ujerumani), Istanbul Basaksehir (Uturuki)
  KUNDI D: AC Milan (Italia), Austria Vienna (Austria), Rijeka (Croatia), AEK Athens (Ugiriki)
  KUNDI E: Lyon (Ufaransa), Everton (England), Atalanta (Italia), Apollon (Cyprus)
  KUNDI F: Copenhagen (Denmark), Lokomotiv Moscow (Urusi), Sheriff (MDA), Zlin (Jamhuri ya Czech)
  KUNDI G: Victoria Plzen (Jamhuri ya Czech), Steaua Bucharest (Romania), Hapoel Beer-Sheva (Isreal), Lugano (Uswisi)
  KUNDI H: Arsenal (England), BATE Borisov (Bulgaria) Cologne (Ujerumani), Red Star Belgrade (Serbia)
  KUNDI I: Salzburg (Austria) Marseille (Ufaransa) Vitoria SC (Ureno) Konyaspor (Uturuki)
  KUNDI J: Athletic Bilbao (Hispania), Hertha Berlin (Ujerumani), Zorya (Ukraine), Ostersund (Sweden)
  KUNDI K: Lazio (Italia), Nice (Ufaransa), Zulte Waregem (Ubelgiji), Vitesse (Uholanzi)
  KUNDI L: Zenit St Petersberg (Urusi), Real Sociedad (Hispania), Rosenborg (Norway), Vardar (Macedonia) 

  Kocha Mfaransa wa Arsenal, Arsene Wenger amepangwa kundi gumu Ligi ya Ulaya pamoja na FC Cologne ya Ujerumani  PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  TIMU za Arsenal na Everton zimepangwa makundi tofauti katika Ligi ya Ulaya msimu wa 2017-18 Europa League baada ya droo iliyofanyika mjini Monaco leo.
  The Gunners wamepangwa pamoja na mabingwa wa Belarus, Bate Borisov, Cologne ya Ujerumani na Red Star Belgrade ya Serbia katika Kundi H, wakati Everton imepangwa Kundi E pamoja na Lyon ya Ufaransa, Atalanta BC ya Italia na Apollon Limassol ya Cyprus.
  Timu ya Arsene Wenger imejikuta nje ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza ndani ya miongo miwili, lakini ni miongoni mwa timu zinazopewa nafasi kubwa ya kushida taji hili mjini Lyon, Ufaransa mwezi Mei mwakani. 
  Everton nayo inatarajiwa kufanya vizuri kwenye michuano hiyo ya Ulaya baada ya kurejea kwa shujaa wake, Wayne Rooney atakayejaribu kutwaa tena taji alilolitwaa na Manchester United msimu uliopita. 
  Katika droo hiyop, vigogo wengine wa Ulaya, AC Milan wamepangwa Kundi D pamoja Austria Wien, AEK Athens na mabingwa wa Croatia, Rijeka.
  Hoffenheim, ambayo ilitolewa na Liverpool katika mchujo wa kuwania kwenda hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, imepangwa Kundi C pamoja na Sporting Braga, Ludogorets na Istanbul Basaksehir.
  Kundi K linazikutanisha na Lazio na Nice, wakati Real Sociedad imepangwa na mabingwa wa Urusi, Zenit St. Petersburg katika Kundi L. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YAPANGWA NA FC COLOGNE, BATE LIGI YA ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top