• HABARI MPYA

  Tuesday, August 22, 2017

  PACQUIAO KURUDIANA NA JEFF HORN AUSTRALIA NOVEMBA

  IMETHIBITISHWA Manny Pacquiao atakuwa na pambano la marudiano na Jeff Horn mjini Brisbane, Australia baadaye mwaka huu.
  Tajiri wa Brisbane, Meya Graham Quirk awali alishutumiwa kutoa taarifa bila uthibitisho kutoka kambi ya Pacquiao, lakini sasa amesema kwamba amehakikishiwa hilo katika kikao cha Jumatatu na promota wake.
  "Nilikuwa na kikao mapema leo (jana) ambacho kimrthibitisha kwamba Manny Pacquiao atakuja mjini Brisbane mwaka huu kwa pambano la marudiano na Jeff Horn," amesema Quirk.
  Manny Pacquiao amethibitisha kurudiana na Jeff Horn mjini Brisbane baadaye mwaka huu PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  Pambano linatarajiwa kufanyika Novemba pale pale Uwanja wa Suncorp ambako watu 50,000 walimshuhudia mwalimu wa zamani wa shule, Horn akimshinda kwa pointi Pacquiao kwenye pambano la raundi 12 kuwania taji la WBO uzito wa Welter.
  Pacquiao alikataa matokeo hayo akidai mpinzani wake alipendelewa, lakini baadaye likaundwa jopo la wataalamu kupitia upya pambano hilo ili kujua mshindi halali, lakini ikathibitika bondia wa Ufilipino alipoteza pambano kihalali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PACQUIAO KURUDIANA NA JEFF HORN AUSTRALIA NOVEMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top