// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KOCHA TWIGA STARS AENDA MASOMONI UJERUMANI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KOCHA TWIGA STARS AENDA MASOMONI UJERUMANI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Sunday, August 27, 2017

  KOCHA TWIGA STARS AENDA MASOMONI UJERUMANI

  Na Mwandishi Wetu, DARES SALAAM
  KOCHA Msaidizi wa timu ya soka ya taifa ya wanawake, Twiga Stars, Edna Lema yuko nchini Ujerumani kwa mafunzo zaidi ya ufundishaji soka.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online kwa simu kutoka Frankfurt, Ujerumani jana, Edna ambaye ni mchezaji wa zamani wa Twiga Stars amesema kwamba kozi anayoshiriki imeandaliwa na Shirikisho la Soka Ujerumani.  
  “Nipo hapa Frankfurt ninaendelea na kozi hii nzuri sana, ambayo niliomba nafasi mimi mwenyewe katika moja ya jitihada za kujiendeleza kitaaluma,”amesema Edna na kuongeza.
  Edna Lema akiwa Uwanja wa Commerzbank-Arena mjini Frankfurt, Ujerumani
  Edna Lema akiwa na washiriki wenzake wa kozi huyo
  Akiwa njiani kwenda Ujerumani, Edna
  alikutana na Mwanasoka Bora wa zamani
  Afrika, Mcameroon Rogger Milla
  “Walihitaji kocha ambaye pia aliwahi kuwa mchezaji, hivyo ikawa bahati yangu mimi kupata nafasi hii na huku nimekutana na makocha wengine ambao walikuwa wachezaji pia wakati wao,”amesema.
  Edna amesema kwamba kiu yake ni kujiendeleza zaidi kielimu ili awe kocha wa kike wa kiwango cha juu baadaye aje kuisaidia nchi yake. Na ametoa wito kwa wachezaji wengine wa zamani wa timu ya taifa kugeukia elimu ya ukocha ili waweze kurithisha ujuzi wao kwa kizazi kipya.
  Umaarufu wa Edna Lema ulianzia wakati anachezea timu ya Polisi Moro mwaka 2000 hadi 2002 alipohamia Mchangani Sisters. Na aliichezea timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania, Twiga Stars kuanzia mwaka 2001 hadi mwaka 2006 alipostaafu na kuanza kuchukua mafunzo ya ukocha kabla ya kuwa kocha Msaidizi wa Twiga Stars.  

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KOCHA TWIGA STARS AENDA MASOMONI UJERUMANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top