// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); BANDA AINUSURU BAROKA KUPIGWA NA MICHO NYUMBANI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE BANDA AINUSURU BAROKA KUPIGWA NA MICHO NYUMBANI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Tuesday, August 22, 2017

  BANDA AINUSURU BAROKA KUPIGWA NA MICHO NYUMBANI

  Na Mwandishi Wetu, JOHANNESBURG
  BEKI Mtanzania, Abdi Hassan Banda leo ameinusuru timu yake mpya, Baroka FC kulala nyumbani mbele ya Orlando Pirates ya kocha Mganda, Milutin Sredojevic ‘Micho’ baada ya kuifungia bao la kusawazisha katika sare ya 1-1.
  Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya ABSA Afrika Kusini uliofanyika Uwanja wa Peter Mokaba mjini Johannesburg, Banda aliyejiunga na timu hiyo mwezi Juni akitokea Simba ya Tanzania, alifunga bao hilo dakika ya 73 kwa kichwa kufuatia mpira wa kona ya juu juu.
  Abdi Banda leo ameinusuru Baroka FC kulala nyumbani mbele ya Orlando Pirates katika mechi ya Ligi Kuu ya ABSA Afrika Kusini

  Hilo lilikuwa bao lililowazuia Pirates kuondoka pointi tatu Uwanja wa Peter Mokaba, baada ya Thabo Qalinge kuifungia The Buccaneers bao la kuongoza dakika ya 41. 
  Vikosi vilikuwa; Baroka FC: Vries; Kgoetyane/Mothupa dk16, Mahashe, Banda, Masenamela - Chawapiwa, Madubanya, Mosele/Mdatsane dk45+4, Kgaswane, Moeti na Motupa/Ntshangase dk47.
  Orlando Pirates: Sandilands; Shitolo, Nyauza, Matlaba, Maela – Mobara/Nkosi dk82, Makola, Nyatama, Memela/Rakhale dk59, Qalinge/Kutumela dk80 na Gabuza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BANDA AINUSURU BAROKA KUPIGWA NA MICHO NYUMBANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top