• HABARI MPYA

  Thursday, August 24, 2017

  MESSI AWASILI KWA HELIKOPTA KWENYE 'TUZO YA RONALDO'

  NYOTA wa Barcelona, Lionel Messi amewasili mjini Monaco, Ufaransa leo kwa helikopta kushiriki zoezi la upangaji wa makundi na ratiba ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
  Messi ataiwakilisha timu yake, Barcelona, ambayo itahusika katika upangaji wa makundi na ratiba ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
  Lakini sababu kubwa ya Muargentina huyo kuhudhuria zoezi hilo ni kwamba amejumuishwa kwenye orodha ya mwisho ya wachezaji watatu wanaowania tuzo ya Mwanasoka Bora wa Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA).
  Wapinzani wa Messi katika Tatu Bora hiyo ni kipa wa Juventus, Gianluigi Buffon na mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo.

  Lionel Messi baada ya kuwasili mjini Monaco, Ufaransa kwa ajili ya tuzo za Mwanasoka Bora wa UEFA
   
  PICHA ZOTE GONGA HAPA 

  Licha ya kufunga mabao 11 na kuseti mawili katika mechi tisa za Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita, Messi hatarajiwi kushinda tuzo hiyo.
  Ronaldo anatarajiwa kutetea tuzo hiyo aliyotwaa miezi 12 iliyopita, baada ya msimu mwingine mzuri akitwaa mataji matatu, la Ligi ya Mabingwa, La Liga na Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA akiwa na Real.
  Buffon pia alikuwa ana msimu mzuri wa 2016-2017, kakidaka mechi mbili bila kuruhusu nyavu zake kutikisika akiiwezesha Juventus kuitoa Barca katika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa.
  Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 39 ametwaa mataji mengine mawili ya Serie A na Coppa Italia, lakini hawezi kushinda tuzo ya UEFA kwa sababu Ronaldo ndiye mtarajiwa kwa mafanikio yake ya msimu uliopita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MESSI AWASILI KWA HELIKOPTA KWENYE 'TUZO YA RONALDO' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top