• HABARI MPYA

  Monday, August 21, 2017

  YANGA YAAMUA KUCHANGAMKIA DILI LA JEZI, YAWAITA FARAGHA WAAGIZAJI NA WAUZAJI IJUMAA JANGWANI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  UONGOZI wa Yanga umeitisha mkutano na wafanyabiashara wote wa jezi utakaofanyika Ijumaa wiki hii makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam.
  Ofisa Mawasiliano wa klabu ya Yanga, Dissmas Ten amesema katika taarifa ya leo jioni kwamba pamoja na kuitisha mkutano huo, wanapiga marufuku mara moja kwa mtu yeyote kuuza jezi yenye nembo ya klabu hiyo kuanzia kesho.
  “Yanga inatoa tahadhari kwa watu wote ambao kwa namna moja au nyingine watashiriki kuuza  au jezi zenye nembo ya Yanga kuanzia kesho watakamatwa na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao,”imesema taarifa hiyo.
  Hizi ndizo jezi rasmi za msimu za nyumbani na ugenini za Yanga SC
  Ten amesema kwamba kikosi maalum kimeandaliwa kufanya ukaguzi na ufuatiliaji wa jambo hilo na kwamba wahujumu wote watakamatwa.
  Hatua hii inamaanisha sasa Yanga wanaelekea kuanza kujiendesha kibiashara, baada ya muda mrefu wa kushindwa kutumia fursa ya rasilimali watu iliyonayo kujinufaisha kimapato. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAAMUA KUCHANGAMKIA DILI LA JEZI, YAWAITA FARAGHA WAAGIZAJI NA WAUZAJI IJUMAA JANGWANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top