// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MAN U YAPANGWA NA BENFICA, SPURS NA CHELSEA MADRID - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MAN U YAPANGWA NA BENFICA, SPURS NA CHELSEA MADRID - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Thursday, August 24, 2017

  MAN U YAPANGWA NA BENFICA, SPURS NA CHELSEA MADRID

  TIMU ya Tottenham Hotspur ya England imepangwa kundi gumu, H katika Ligi ya Mabingwa Ulaya pamoja na mabingwa watetezi, Real Madrid ya Hispania na mabingwa wa zamani, Borussia Dortmund ya Ujerumani.
  Klabu zote Manchester na Liverpool zimepata makundi mepesi wakati Chelsea pamoja na kupangwa kundi moja na timu ya kocha, Diego Simeone, Atletico Madrid pia inapewa nafasi ya kufuzu.
  Wakati huo huo, Celtic ya Scotland imewekwa pagumu baada ya kupangwa na mabilionea, PSG ya Ufaransa, mabingwa wa zamani Bayern Munich ya Ujerumani na Anderlecht ya Ubelgiji katika Kundi B.
  Kundi D lina mabingwa wawili wa zamani, Juventus ya Italia ambao pia ni washindi wa pili wa msimu uliopita, Barcelona ya Hispania, Olympiacos ya Ugiriki na Sporting Lisbon Ureno.

  Real Madrid wakifurahia na taji lao la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita baada ya kuifunga Juventus mwezi Mei mwaka huu PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  KUNDI A 

  Benfica (Ureno) 
  MANCHESTER UNITED (England) 
  Basle (Uswisi) 
  CSKA Moscow (Urusi) 

  KUNDI B 

  Bayern Munich (Ujerumani) 
  PSG (Ufaransa) 
  Anderlecht (Ubelgiji) 
  Celtic (Scotland) 

  KUNDI C 

  CHELSEA (England)
  Atletico Madrid (Hispania) 
  Roma (Italia) 
  Qarabag (Azerbaijan) 

  KUNDI D 

  Juventus (Italia) 
  Barcelona (Hispania) 
  Olympiacos (Ugiriki) 
  Sporting Lisbon (Ureno) 

  Kundi E 

  Spartak Moscow (Urusi) 
  Sevilla (Hispania) 
  LIVERPOOL (England) 
  Maribor (Slovenia) 

  KUNDI F 

  Shakhtar Donetsk (Ukraine) 
  MANCHESTER CITY (England) 
  Napoli (Italia) 
  Feyenoord (Uholanzi) 

  KUNDI G 

  Monaco (Ufaransa) 
  Porto (Ureno) 
  Besiktas (Uturuki) 
  RB Leipzig (Ujerumani) 

  KUNDI H 

  Real Madrid (Hispania) 
  Borussia Dortmund (Ujerumani) 
  TOTTENHAM (England) 
  Apoel (Cyprus) 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN U YAPANGWA NA BENFICA, SPURS NA CHELSEA MADRID Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top