• HABARI MPYA

  Thursday, August 24, 2017

  WAYNE ROONEY AAMUA KUSTAAFU SOKA YA KIMATAIFA

  MSHAMBULIAJI wa Everton, Wayne Rooney amestaafu kuchezea timu ya taifa ya England jana, ikiwa ni wiki chache tu baada ya kusema anataka kucheza fainali zijazo za Kombe la Dunia.
  Mfungaji huyo bora wa jumla wa nchi hiyo, ametoa tamko la kushitua kwa kutangaza kustaafu siku moja kabla ya kocha Gareth Southgate kutaja kikosi cha England kwa ajili ya mechi zijazo dhidi ya Malta na Slovakia.
  Uamuzi huo utakapokewa kwa mshangao na mashabiki wa England na Southgate na itachukuliwa kama Rooney hakufurahia uhamisho wa kutoka Manchester United kurejea Everton mwezi uliopita, ambako alikuwa ana matumaini ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia Urusi.
  Wayne Rooney amestaafu kuchezea England baada ya kutangaza hayo jana GONGA HAPA KUSOMA ZAIDI 

  WAFUNGAJI BORA WA KIHISTORIA ENGLAND

  Wayne Rooney 53
  Bobby Charlton 49
  Gary Lineker 48
  Jimmy Greaves 44
  Michael Owen 40
  Tom Finney 30
  Nat Lofthouse 30
  Alan Shearer 30 
  Southgate aliamua kumuita tena kikosini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 baada ya kumuona akifunga bao lake la pili dhidi ya Manchester City katika Ligi Kuu ya England kwenye mechi ya pili mfululizo Jumatatu usiku. 
  Kocha huyo wa England aliamua kumfahamisha Rooney juzi kwamba atakuwemo kwenye kikosi chake, lakini mshambuliaji huyo akampigia Southgate kumuambai ameamua kustaafu soka ya kimataifa.
  "Ni maamuzi magumu na ambayo nilijadiliana na familia yangu, kocha wangu wa Everton na watu wangu wa karibu,"amesema Rooney na kuongeza; "Kucheza England wakati wote kimekuwa kitu maalum kwangu,". 
  "Wakati wote nilipoteuliwa kama mchezaji au Nahodha ilikuwa ni kipaumbele na ninamshukuru kila mmoja aliyenisaidia. Lakini naamini sasa ni wakati wa kujitoa,".
  Rooney amefunga mabao 53 katika timu ya taifa ya England tangu alipoibuka kwa mara ya kwanza akiwa ana umri wa miaka 17 tu katika mchezo dhii ya Australia mwaka 2003.
  Lakini nafasi yake kwenye kikosi cha England imeanza kupungua kwa miezi 12 iliyopita kutokana na kuanza kupotea kwenye kikosi cha kwanza cha United.
  Mshambulaiji chaguo la kwanza wa England kwa sasa, Harry Kane ndiye anatarajiwa kuw Nahodha wa muda mrefu wa timu. Ikumbukwe, Southgate aliyechukua nafasi ya Roy Hodgson na Sam Allardyce katika kujilazimisha kumtumia Rooney, alikuwa anamtumia katika safu ya kiungo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WAYNE ROONEY AAMUA KUSTAAFU SOKA YA KIMATAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top