• HABARI MPYA

    Saturday, August 26, 2017

    MAYANGA AWAREJESHA YONDAN NA MWADINI TAIFA STARS

    Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
    KOCHA wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars amemrejesha kikosini beki mkongwe na 'mtukutu' wa Yanga, Kevin Yondan kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Botswana wiki ijayo.
    Yondan amekuwa na kawaida ya kukaidi wito kwenye kikosi cha Taifa Stars na aliwhai kumgomea kocha Mholanzi, Mart Nooij aliyekuwa anasaidiwa na Mayanga mwaka juzi na baadaye Charles Boniface Mkwasa. 
    Mkwasa baadaye aliamua kuachana na mchezaji huyo wa zamani wa Simba na Mayanga naye baada ya kupewa timu Machi mwaka huu hakumuita, lakini sasa amejaribu tena kuona kama kijana amebadilika.
    Akizungumza na Waandishi wa Habari leo ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Uwanja wa Karume, Dar es Salaam – Mayanga amesema kwamba kwa sababu ya majeruhi hajawaita kipa bora wa michuano ya COSAFA, Said Mohammed Ndunda na mshambuliaji John Raphael Bocco, wote wa Simba.
    Mayanga amesema kwa sababu kama hizo pia hajamuita kipa wa Yanga, Beno Kakolanya kwa ajili ya maandalizi mchezo wa kirafiki dhidi ya Botswana Septemba 2, mwaka huu Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na badala yake amemrejesha Mwadini Ali wa Azam.
    'Mtukutu' Kevin Yondan ameitwa tena Taifa Stars kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Botswana wiki ijayo

    Kwa ujumla kikosi kamili cha Stars alichoteua Mayanga kinaundwa na makipa; Aishi Manula (Simba), Mwadini Ali (Azam FC) na Ramadhani Kabwili (Yanga SC).
    Mabeki; Gardiel Michael (Yanga), Boniface Mganga (Mbao FC), Abdi Banda (Baroka FC, Afrika Kusini), Kelvin Yondan (Yanga), Salim Mbonde (Simba) na Erasto Nyoni (Simba).
    Viungo; Himid Mao (Azam FC), Hamisi Abdalla (Sony Sugar, Kenya), Muzamil Yassin (Simba), Said Ndemla (Simba), Simon Msuva (Difaa Hassan El- Jadida, Morocco), Shiza Kichuya (Simba), Farid Mussa (Tenerrife B, Hispania) na Morel Ergenes (FC Famalicao/Ureno).
    Washambuliaji; Rafael Daudi (Yanga), Kelvin Sabato (Mtibwa Sugar), Mbwana Samatta (KRC Genk, Ubelgiji) na Elius Maguli (Dhofar FC, Oman).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAYANGA AWAREJESHA YONDAN NA MWADINI TAIFA STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top