• HABARI MPYA

  Wednesday, August 23, 2017

  NJE YA LIGI KUU, SIMBA WAMEITESA ZAIDI YANGA

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  NJE ya mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba na Yanga zimekuwa zikikutana katika mechi zenye msisimko wakati mwingine za kuwania mataji, tena yenye thamani ya mamilioni na mvuto wake umebaki kuwa kama kawaida.
  Kwa wenye kuikumbuka mechi ya fainali ya Ligi, Uwanja wa Nyamagana, mjini Mwanza mwaka 1974, hawawezi kuisahau mechi ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, kwa sasa maarufu kama Kombe la Kagame.
  Kwa nini? Kwa sababu wafungaji wa mabao ya Yanga kwenye Uwanja wa Nyamagana ndio wafungaji wa mabao wa timu hiyo katika ushindi wa 2-0 visiwani Zanzibar kwenye Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati. 
  Hiyo ilikuwa mechi ya kwanza kubwa kuzikutanisha Simba na Yanga nje ya Ligi Kuu na Watoto wa Jangwani, chini ya kocha kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wakati huo wakaibuka na ushindi wa mabao 2-0 na kutwaa Kombe.
  Tangu wakati huo, watani hao wa jadi katika soka ya Tanzania wamekutana kwenye mechi ambazo si za Ligi mara 22 na katika hizo, Yanga imeshinda mechi tisa, Simba mechi 11 na zimetoka sare mara mbili. 
  Hiyo ni nje ya pambano kuwania nafasi ya tatu Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati Julai 27, mwaka 2008, ambalo Yanga haikutokea Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Simba ikapewa ushindi wa chee.
  Zifuatazo ni mechi zite za Simba na Yanga nje ya Ligi Kuu.
  Kutoka kulia, Mganda Emmanuel Okwi, Mkongo marehemu Patrick Muteesa Mafisango na Mzambia Felix Sunzu wakifurahia ushindi wa 2-0 dhidi ya Yanga katika mechi ya Ngao ya Jamii Agosti 17, mwaka 2011 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

  REKODI YA SIMBA NA YANGA NJE YA LIGI KUU:
                          P W D L Pts 
  Simba SC 22 11 2 9 35
  Yanga SC 22 9 2 11 29

  NANI MTANI JEMBE:
  DESEMBA 13, 2014
  Simba SC 2-0 Yanga
  WAFUNGAJI:
  SIMBA SC: Awadh Juma na Elias Maguri 
  NANI MTANI JEMBE:
  DESEMBA 23, 2013
  Simba SC 3-1 Yanga
  WAFUNGAJI:
  SIMBA SC: Amisi Tambwe dk 14 na 44penalti na Awadh Juma dk, 
  YANGA SC: Emmanuel Okwi dk87  
  KLABU BINGWA AFRIKA MASHARIKI NA KATI:
  JULAI 10, 2011
  Yanga 1-0 Simba, Fainali 
  MFUNGAJI : Kenneth Asamoah dk 108 
  JANUARI 1975
  Yanga Vs Simba; Fainali, 2-0
  WAFUNGAJI: Gibson Sembuli na Sunday Manara
  JANUARI 1992
  Simba Vs Yanga; Fainali 
  1-1, Simba ilishinda kwa penalti 5-4
  JULAI 27, 2008
  Simba Vs Yanga; Mshindi wa Tatu
  (Yanga haikutokea uwanjani, Simba ikapewa ushindi wa chee)
  KOMBE LA HEDEX:
  JUNI 30, 1996
  Yanga Vs Simba 2-0
  CCM Kirumba, Mwanza
  WAFUNGAJI: Bakari Malima na Edibily Lunyamila
  KOMBE LA HEDEX:
  JULAI 13, 1996
  Simba Vs Yanga 1-1, Taifa, Dsm
  WAFUNGAJI:
  SIMBA: Hussein Amaan Marsha kwa penalti
  YANGA: Bakari Juma Malima 
  KOMBE LA TUSKER:
  FEBRUARI 10, 2001
  Yanga Vs Simba (fainali) 0-0
  (Simba ilishinda kwa penalti 5-4, Uwanja wa Taifa)
  MACHI 31, 2002.
  Simba Vs Yanga 4-1
  WAFUNGAJI:
  SIMBA: Mark Sirengo dk. 3 na 76, Madaraka Selemani dk. 32 na Emanuel Gabriel dk. 83.
  YANGA: Sekilojo Chambua dk 16.
  (Mechi hii ya fainali iliyohudhuriwa na rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, chupuchupu ivunjike dakika ya 32, baada ya Madaraka kufunga bao ambalo kabla ya kufumua shuti lililomshinda kipa Manyika Peter, aliushika mpira kwa makusudi, ili kuuweka sawa. Rais wa Yanga wakati huo, Tarimba Abbas aliinuka na kuwaonyesha ishara wachezaji wake watoke uwanjani na hapo ndipo meza kuu aliyokuwa ameketi mzee Mwinyi, ilipoanza kushambuliwa kwa chupa za maji na mashabiki wa Yanga. Mwamuzi wa mchezo huo, Abdulkadir Omar alisubiri hadi vurugu zilipotulizwa na FFU ndipo akaendeleza mchezo. Tarimba alitoka nje na hakutaka kuendelea kushuhudia mchezo huo. Baada ya hapo, alifungiwa na Chama cha Soka Tanzania, FAT).
  JULAI 2, 2005
  CCM Kirumba, Mwanza. Fainali
  Simba Vs Yanga, 2-0
  WAFUNGAJI: Emmanuel Gabriel dk. 60, Mussa Hassan Mgosi dk. 72
  AGOSTI 15, 2006
  Simba Vs Yanga; Nusu Fainali, 1-1
  WAFUNGAJI:
  SIMBA: Emanuel Gabriel dk. 69 
  YANGA: Credo Mwaipopo 90
  (Simba ilishinda kwa mikwaju ya penalti 7-6)
  DESEMBA 24, 2009
  Yanga Vs Simba; Nusu Fainali, 2-1 
  WAFUNGAJI: 
  YANGA: Jerry Tegete dk 67, Shamte Ally dk 120
  SIMBA: Hillary Echesa dk 78 (penalti)
  (Uwanja wa mpya wa Taifa)
  KOMBE LA MAPINDUZI:
  Januari 10, 2017; Nusu Fainali
  Simba 0-0 Yanga 
  Simba ilishinda kwa penalti 4-2 
  JANUARI 12, 2011
  Simba Vs Yanga; Fainali 2-0
  WAFUNGAJI: Mussa Mgosi dk 33, Shijja Mkinna dk 71
  (Uwanja wa Amaan, Zanzibar)
  KOMBE LA AICC:
  JUNI 1989
  Yanga Vs Simba SC 1-0
  MFUNGAJI: Joseph Machella 
  APRILI 20, 2003, 
  CCM Kirumba, Mwanza
  Yanga Vs Simba 3-0
  WAFUNGAJI:
  Kudra Omary dk. 30, Heri Morris dk 32 na Salum Athumani dk. 47
  KOMBE LA CCM
  JANUARI 19, 2003
  Simba Vs Yanga 1-1, Dsm
  WAFUNGAJI:
  SIMBA: Jumanne Tondolo dk. 10
  YANGA: Mwinyi Rajabu dk. 20
  NGAO YA JAMII:
  FEBRUARI 17, 2001
  Yangs Vs Simba 2-1, Dsm
  WAFUNGAJI: 
  YANGA: Edibilly Lunyamila dk. 47, AllyYussuf 'Tigana' dk 80.
  SIMBA: Steven Mapunda 'Garrincha' dk.43
  AGOSTI 18, 2010
  Yanga vs Simba 0-0
  (Yanga ilishinda kwa penalti 3-1)
  WAFUNGAJI: Geoffrey Bonny, Stefano Mwasyika na Isaac Boakye kwa upande wa Yanga na Mohamed Banka kwa Simba.
  WALIOKOSA: Ernest Boakye kwa Yanga na Emanuel Okwi, Uhuru Suleiman na Juma Nyosso kwa Simba.
  AGOSTI 17, 2011
  Simba vs Yanga 2-0, Dar 
  WAFUNGAJI:
  Haruna Moshi ‘Boban’ dk 15 na Felix Sunzu dk 38.
  KOMBE LA FAT
  NOVEMBA 15, 2000
  Yanga Vs Simba 2-1
  Sheikh Amri Abeid, Arusha.
  WAFUNGAJI:
  YANGA: Aziz Hunter 40 na Vincent Tendwa
  SIMBA: Ally Yussuf 'Tigana' dk.37
  NOVEMBA 12,  2000
  MARUDIANO KOMBE LA FAT
  Simba Vs Yanga 1-0, Dsm
  MFUNGAJI:
  SIMBA: Ben Luoga  dk.44        
  (Matokeo ya jumla yakawa 2-2 na Yanga ikatolewa kwa mikwaju ya penalti 5-4)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NJE YA LIGI KUU, SIMBA WAMEITESA ZAIDI YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top