// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIBOMANA AUMIA BELARUS, ATAKAA NJE MIEZI MITATU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIBOMANA AUMIA BELARUS, ATAKAA NJE MIEZI MITATU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Tuesday, August 22, 2017

  SIBOMANA AUMIA BELARUS, ATAKAA NJE MIEZI MITATU

  Na Canisius Kagabo, KIGALI
  KIUNGO wa kimataifa wa Rwanda, Sibomana Patrick anayecheza klabu Shakhtyor Soligorsk ya Belarus atakuwa nje kwa miezi miwili kufuatia kuvunjika vidole vya mguu.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online jana kwa simu kutoka Belarus, Sibomana alisema kwamba aliumia jumapili katika mchezo baina ya timu yake na Dinamo Brest uliomalizika kwa sare ya 2-2.
  Na amesema majanga hayo yalimpata wakati anampiga chenga beki mmoja wa Dinamo ambaye alicheza rafu iliyomsababishia maumivu hayo. 
  Patrick Sibomana akiichezea Shakhtyor Soligorsk ya Belarus kabla ya kuumia katika picha ya chini
  “Ndiyo nitakuwa nje kwa miezi miwili bila kucheza kwa sababu nimevunjika, baada ya miezi hiyo nitaanza mazoezi kidogo kidogo. Nilikuwa na mpira nikampiga chenga beki na akanikanyaga na mfupa wa kidole cha mguu ukapasuka,” alisema Patrick. 
  Na Sibomana anaumia katika mechi ya pili tu kuchezea timu hiyo Shakhtyor Soligorsk kufuatia kusajiliwa mapema Agosti kutoka APR ya nyumbani, Rwanda.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIBOMANA AUMIA BELARUS, ATAKAA NJE MIEZI MITATU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top