// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); OMOG AWAANZISHA PAMOJA, MAVUGO, OKWI, NIYONZIMA NA KICHUYA, HUKO YANGA SASA... - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE OMOG AWAANZISHA PAMOJA, MAVUGO, OKWI, NIYONZIMA NA KICHUYA, HUKO YANGA SASA... - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Wednesday, August 23, 2017

  OMOG AWAANZISHA PAMOJA, MAVUGO, OKWI, NIYONZIMA NA KICHUYA, HUKO YANGA SASA...

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KOCHA Mcameroon wa Simba, Joseph Marius Omog amewaanzisha pamoja katika safu ya ushambuliaji Shiza Kichuya, Mnyarwanda Haruna Niyonzima, Mganda Emmanuel Okwi na Mrundi, Laudit Mavugo katika mchezo wa Ngao ya Jamii jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Mchezo huo unatarajiwa kuanza Saa 11:00 jioni utachezeshwa na marefa wa Dar es Salaam Heri Sasii atakayesaidiwa na Hellen Mduma na Ferdinand Chacha wa Mwanza.
  Haruna Niyonzima ameanzishwa pamoja na Emmanuel Okwi na Laudit Mavugo leo

  Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu uliopita, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ ameanzia benchi na kwenye beki ya kushoto leo amepangwa Erasto Nyoni, wakati kulia anaanza Ally Shomary na mlinda mlango ni Aishi Manula.
  Mabeki wa kati ni Salim Mbonde na Mzimbabwe, Method Mwanjali watakaocheza pamoja na kiungo wa ulinzi, James Kotei na kiungo mchezeshaji Muzamil Yassin.
  Kwa ujumla kikosi kamili cha Simba leo ni; Aishi Manula, Ally Shomari, Erasto Nyoni, Salim Mbonde, Method Mwanjale, James Kotei, Shiza Kichuya, Mzamiru Yassin, Laudit Mavugo, Emanuel Okwi na Haruna Niyonzima.
  Katika benchi wapo; Emmanuel Mseja, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Juuko Murshid, Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto, Juma Luizio na Mohammed ‘Mo’ Ibrahim.
  Yanga SC; Youthe Rostand, Juma Abdul, Gardiel Michael, Andrew Vincent ‘Dante’, Kevin Yondan, Papy Kabamba Tshishimbi, Raphael Daudi, Thabani Kamusoko, Ibrahim Hajib, Donald Ngoma na Emmanuel Martin.

  Katika benchi wapo Ramadhan Kabwili, Hassan Kessy, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Mwinyi Mngwali, Said Juma ‘Makapu’, Yussuf Mhilu na Juma Mahadhi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: OMOG AWAANZISHA PAMOJA, MAVUGO, OKWI, NIYONZIMA NA KICHUYA, HUKO YANGA SASA... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top