• HABARI MPYA

  Monday, August 21, 2017

  BURKINA FASO YAITUPA NJE GHANA CHAN 2018 KENYA

  TIMU ya Burkina Faso imeichapa mabao Ghana mabao 2-1 Jumapili na kufuzu Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), inayohusisha timu zinazocheza Ligi za nchini mwao pekee.
  Ghana, walioshika nafasi ya pili mara mbili katika fainali nne zilizopita za michuano hiyo, waliongoza mara mbili nchini Burkina Faso wikiendi iliyopita kabla ya kufungwa bao la dakika za mwishoni na kumaliza kwa sare ya 2-2 kwenye mchezo wa kwanza.
  Faida ya kucheza nyumbani mjini Kumasi – nyumbani kwa klabu maarufu nchini humo, Asante Kotoko – ilitarajiwa kuibeba Ghana na kufuzu kwenye fainali hizo kwa mara ya nne.
  Lakini wenyeji waliduwazwa na Burkinabe walionufaika na mabao ya Mohammed Sylla na Herman Nikiema ndani ya dakika 30 Uwanja wa Baba Yaro. Felix Addo alifunga bao la kufutia machozi la Ghana.
  Burkina Faso imefuzu kwa ushindi wa jumla wa 4-3 na itaungana na nchi nyingine 15 kwenye michuano hiyo itakayofanyika Kenya kuanzia Januari 12 hadi Februari 4. 
  Nchi zilizofuzu hadi sasa ni wenyeji Kenya, Angola, Cameroon, Kongo, Ivory Coast, Equatorial Guinea, Libya, Morocco, Nigeria, Sudan, Zambia na Namibia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BURKINA FASO YAITUPA NJE GHANA CHAN 2018 KENYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top