• HABARI MPYA

  Saturday, August 26, 2017

  NIYONZIMA: SIMBA NAJIONA KAMA NIMEZALIWA UPYA

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  WAKATI Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuanza leo, kiungo mpya wa Simba, Mnyarwanda Haruna Niyonzima amesema kwamba anajiona kama amezaliwa upya baada ya kuhama timu.
  Haruna ameondoka Yanga alikodumu kwa miaka sita tangu mwaka 2012 na kujiunga na mahasimu, Simba msimu huu.
  Na akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online jana, Haruna amesema kwamba kuhama timu kwa hamasa kubwa kunamuhamasisha mchezaji kujibidiisha ili kufanya vizuri.
  “Unajua nimeondoka Yanga walikuwa bado wanahitaji kuwa na mimi, nimekuja huku ambako nako walikuwa wananihitaji sana. Ni jambo zuri, lakini ni changamoto kubwa kwa mchezaji. Ona mimi sasa, najiona kama nimezaliwa upya kwa sababu kila kitu ni kipya mbele yangu. Utamaduni ni tofauti na ule niliuzoea kwa miaka sita iliyopita,”amesema.
  Haruna Niyonzima amesema kwamba anajiona kama amezaliwa upya baada ya kuhamia Simba

  Niyonzima amesema uhamisho huu wa rekodi katika historia yake unamfanya lazima ajibidiishe kufanya vizuri ili kumfurahisha kwanza mwajiri wake, lakini pia na kuendelea kukuza heshima yake katika soka ya Tanzania.
  “Mpira kwangu ni kazi, ninapaswa kuwa fiti wakati wote ili kucheza vizuri na kuendelea kuweka heshima yangu, kumfurahisha mwajiri wangu na mashabiki pia wale wanakuja kwa wingi kumuona Haruna na timu katika kila mechi,”amesema. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NIYONZIMA: SIMBA NAJIONA KAMA NIMEZALIWA UPYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top