• HABARI MPYA

  Friday, August 25, 2017

  SIMBA NA RUVU, YANGA NA LIPULI KUPIGWA SHAMBA LA BIBI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MICHEZO ya ufunguzi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inayozihusisha timu za Dar es Salaam itachezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, maarufu kama Shamba la Bibi kutokana na Uwanja wa Taifa kuingia kwenye programu ya upandikizaji upya wa nyasi.
  Msimu mpya wa Ligi Kuu wa 2017/2018 unaanza rasmi Jumamosi y Agosti 26, 2017 kwa michezo saba itayochezwa katika viwanja tofauti nchini kutafuta bingwa atakayeshiriki pia Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2019.
  Kwa mechi za kesho Jumamosi, Simba inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Ruvu Shooting katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam wakati Mbao watakuwa wageni wa Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
  Mchezo mwingine utakuwa ni kati ya Majimaji ya Songea itakayosafiri hadi Mbeya kucheza na Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine jijini humo huku Njombe Mji ikiialika Tanzania Prisons ya Mbeya kwenye Uwanja wa Sabasaba huko Makambako.
  Kadhalika Uwanja wa Manungu ulioko Turiani, Mtibwa mkoani Morogoro, Mtibwa Sugar itaikaribisha Stand United ya Shinyanga kwenye mchezo mwingine wa VPL ilihali Azam atakuwa mgeni wa Ndanda FC kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara. 
  Mwadui watakuwa wenyeji wa Singida United ya Singida kwenye Uwanja wa Mwadui huko Shinyanga na Jumapili kutakuwa na Mchezo mmoja utakaowakutanisha mabingwa watetezi, Yanga SC dhidi ya Lipuli ya Iringa Uwanja wa Uhuru.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA NA RUVU, YANGA NA LIPULI KUPIGWA SHAMBA LA BIBI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top