• HABARI MPYA

  Sunday, August 20, 2017

  SAMATTA AKWAA KISIKI UBELGIJI, GENK WADUNDWA 1-0 NYUMBANI

  Na Mwandishi Wetu, GENK
  BAADA ya kufanya vizuri katika mchezo uliopita akifunga mabao mawili na kuseti mawili, timu yake, KRC Genk ikishinda 5-3 dhidi ya wenyeji, Royal Antwerp FC katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A nchini humo, Uwanja wa Bosuilstadion, Deurne – jana mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta alikwaa kisiki.
  Hiyo ni baada ya Genk kufungwa 1-0 nyumbani Uwanja wa Luminus Arena na Sporting Charleroi katika mfululizo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji tena kwa bao la kujifunga wenyewe kupitia kwa kiungo Mnorway, Sander Berge.
  Huo unakuwa mchezo wa 59 kwa Samatta katika mashindano tangu Januari mwaka jana alipojiunga na Genk, kati ya hiyo mechi 35 alianza na mechi 21 alitokea benchi.
  Katika mechi hizo, mshambuliaji huyo wa zamani wa African Lyon, zamani Mbagala Market na Simba zote za Dar e Salaam, amefunga jumla ya mabao 21.
  Kikosi cha KRC Genk jana kilikuwa: Vukovic, Khammas, Colley, Brabec, Mata, Berge, Malinovskyi/Ingvartsen dk63, Writers, Trossard/Pozuelo dk68, Buffalo/Benson dk77 na Samatta.
  Charleroi: Penneteau, Martos, Rezaei/Bedia dk88, Pollet/Benavente dk75, Diandy, Marinos, Baby, Dessoleil, Nurio, Ilaimaharitra and Lukebakio/Saglik dk79.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA AKWAA KISIKI UBELGIJI, GENK WADUNDWA 1-0 NYUMBANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top