• HABARI MPYA

    Wednesday, June 01, 2016

    SAMATTA ATUA LEO STARS, MISRI WAFIKIA KEMPINSKI...KAZI IPO JMOSI TAIFA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    NAHODHA wa timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta (pichani kushoto) anatarajiwa kuwasili usiku wa leo kutoka Genk Ubelgiji kujiunga na kambi ya timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars kwa ajili ya mchezo dhidi ya Misri Jumamosi kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani.
    Na Samatta anatua leo, siku mbili baada ya mshambuliaji pacha wake,  Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kujiunga na timu hiyo. 
    Katika hatua nyingine, Uongozi wa Bia ya Kilimanjaro inayozalishwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL), unatarajia kutembelea timu ya Taifa Stars kesho Alhamisi Juni 2, 2016 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa lengo la kuwapa hamasa wachezaji wa timu hiyo kabla ya kuivaa Misri Juni 4, 2016 katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Maataifa ya Afrika (AFCON).
    Mchezo huo utasimamiwa na Waamuzi wanne kutoka Gabon, ambao ni Meye Bastrel atakayesaidiwa na Mihundou Ganther na Vinga Theophile wakati Mwamuzi wa akiba (mezani) atakuwa Otogo Eric. Wakati waamuzi wote wanatoka Gabon, Kamishna wa mchezo huo ni Tarig Atta Salih kutoka Sudan.
    Maandalizi ya mchezo huo yamekamilika kwa Shirikisho Soka la Tanzania (TFF) na Misri imetua alfajiri ya leo Juni 1, 2016 na imeweka kambi kambi kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempiski, Dar es Salaam.
    Taifa Stars imeweka kambi Hoteli Urban Rose ambayo pia iko katikati ya jiji la Dar es Salaam tangu iliporejea kutoka Kenya jana Mei 30,2016 ambako ilicheza timu ya Taifa ya Kenya maarufu kama Harambee Stars. Katika mchezo huo uliofanyika Jumapili Mei 29, mwaka huu timu hizo zilitoka sare ya 1-1.    
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAMATTA ATUA LEO STARS, MISRI WAFIKIA KEMPINSKI...KAZI IPO JMOSI TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top