• HABARI MPYA

  Monday, June 27, 2016

  KAPTENI BOCCO ANAVYOJIFUA KUJIANDAA NA MSIMU MPYA

  Nahodha wa Azam FC, John Raphael Bocco 'Adebayor' akifanya mazoezi ya kukimbia katika ufukwe wa bahari ya Hindi eneo la Africana, Mbezi mjini Dar es Salaam kujiandaa na msimu mpya
  Mshambuliaji huyo ana wiki sasa akifanya mazoezi binafsi kujiweka fiti kabla ya kuingia kwenye programu za maandalizi ya msimu mpya za timu yake
  Bocco amesema asubuhi anafanya mazoezi ufukweni, mchana gym na jioni anacheza mpira na timu ya mtaani kwake
  Bocco amesema nia yake ni kuhakikisha msimu ujao anarejesha makali yake na kuisaidia timu yake
  Ikumbukwe msimu uliopita Bocco hakufanya vizuri sana kutokana na kuandamwa na maumivu
  Bocco pia ni mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania na Nahodha wa kikosi cha CHAN
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAPTENI BOCCO ANAVYOJIFUA KUJIANDAA NA MSIMU MPYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top